Wednesday, December 31, 2014

MWAKYEMBE AMWAGA CHOZI TRL LEO,AFUKUZA MABOSI KIBAO,SOMA HAPA


Pichani ni WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe
akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa Shirikala la reli
(TRL) leo jijini Dar es Salaam


NA KAROLI VINSENT

HUKU ikiwa imebaki Miezi kumi ili Rais Jakaya Kikwete amalize mada wake,Sasa WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ametema Cheche Baada ya leo  Kuibuka na kuwasimamisha pamoja na kuwafukuza kazi watumishi 12 wa Kampuni la Reli Tanzania (TRL), kwa tuhuma za kuhujumu shirika hilo huku akiagiza wachukuliwe hatua za kisheria  pamoja na kufulisiwa.
            
Hatua hiyo ni mwendelezo wa Waziri Mwakyembe kusafisha wafanyakazi wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu, vinavyokwenda kinyume na jitihada za serikali kutaka TRL kujiendesha kwa faida na kuondokana na utegemezi ambao shirika hilo limekuwa mzigo kwa sasa kwa serikali kutokana na ufisadi huo.
  
  Akizungumza na waandishi pamoja na wafanyakazi wa TRL,leo Jijini  Dar es Salaam ,ambapo Waziri Mwakyembe aliwataja wafanyakazi waliofukuzwa kazi ni Stanley Makunja, Stanley Edward, Jason Moses, B. Luoga, Edward Benedict, na Lucy Ntinya ambapo wanadaiwa kugushi malipo ya tiketi za abiria na kuitia hasara TRL.



Wafanyakazi wa Shirika la Reli nchini pamoja na Waaandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Waziri Mwakyembe
     Alisema wafanyakazi hao waligushi malipo ya tiketi za abiria waliokuwa wakisafiri na treni kwenda mikoa mbalimbali nchini ambapo malipo waliolipa abiria hao ni tofauti na malipo yaliyoandikwa kwenye kitabu cha risiti.
    Mwakyembe aliongeza kuwa  wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti waligushi risiti mbalimbali zikiwemo zenye namba 622405 iliyolipiwa sh. 50,200 lakini fedha iliyoingia TRL ni sh 13,600, risiti yenye namba 6224010 iliyolipiwa sh 74,400 huku fedha iliyoingia kwenye kampuni hiyo ni 13,600
     Aidha ,Mwakyembe alitaja risiti yenye namba 622408 iliyolipiwa sh 57,000 ilighushiwa huku TRL ikipata sh 6,700 hivyo alisema kitendo kilichofanywa na wafanyakazi hao hakikubaliki.
      Vilevile, katika mkutano huo, alitangaza kusimamishwa kazi maafisa sita wanaodaiwa kuiisababishia hasara kampuni hiyo kwa kushindwa kuhakiki ubora wa mabehewa ya maizigo yaliyonunuliwa na serikali.
   Waziri Mwakyemba Aliwataja maafisa hao ambao ni waandisi kuwa ni Pascal, Ngoso, Kaukunda, Chambika, Lugela na Kessy ambapo barua zao za kusimamishwa kazi wamekabidhiwa Disemba 10 mwaka huu.
     Alibainisha kuwa pamoja na maamuzi hayo kufikiwa, bodi ya zabuni ya TRL imevunjwa na tayari mchakato wa kuundwa kwa bodi mpya umeanza.
     Katika sakata hilo la ubovu wa mabehewa ya mizigo na kusababisha kuanguka pindi yanapokuwa safarini, Mwakyembe ameunda kamati ya wataalamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), Bodi ya Wahandisi, TRL huku akimuagiza  Katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kuongeza wataalamu wawili kufuatilia ubora wa mabehewa hayo.
       Mwakyembe ambaye pia ni mbunge wa kyela CCM,Alisema kamati hiyo itakwenda nchini India kwenye kampuni ya Hindu Stant kuhakiki ubora wa mabehewa hayo na pindi ikibainika kuwa hayakutengenezwa kulingana na viwango vinavyokubalika basi serikali itachukua hatua za kisheria,
“ Lazima tukahakiki ubora wa mabehewa hayo kwakuwa inashangaza kuona mabehewa mapya pekee ndiyo yana anguka hivyo lazima tufahamu ukweli wa mambo” alisema.
      Katika hatua nyingine Mwakyembe aliitaka bodi ya TRL kusitisha mikataba na kampuni za Translaw, R and A works, Solar security, Kigema security na Intergrated zilizokuwa na mikataba na TRL.
        Alisema kazi zinazofanywa na kampuni hizo zikiwemo kuhesabu idadi ya mizigo inayosafirishwa zinaweza kufanywa na wafanyakazi wa shirika hilo.
       Alisisitiza kuwa madai yanayotolewa na Menejimenti ya TRL kuwa kazi hizo zinahitaji uwepo wa wafanyakazi wengi na wenye ujuzi mbalimbali ikiwemo za ukarani, na ukarabati wa miundombinu ya reli hayana msingi.
          Aidha,Mwakyembe alisema kwa upande wa kampuni za ulinzi ni vyema kazi hiyo ikafanywa na SUMA JKT shirika kwa kuwa wanauwezo wa kuhakikisha vitendo vya wizi vinadhibitiwa.

No comments: