ELIMU BURE--MTATIRO AMGEUKIA RAIS KIKWETE,SOMA ALICHOSEMA HAPA

BW   ;JULIUS  MTATIRO  KADA  WA  CHAMA  CHA  CUF 


SOMA   KAULI  YAKE  HAPA

RAIS KIKWETE ANASEMA KUANZIA MWAKA 2016 CCM ITATOA ELIMU YA SEKONDARI BURE...
Kwa nini aanze kupanga sera za serikali ijayo wakati yeye atakuwa Msoga, kijijini kwake? Na kama yeye ni bingwa wa mipango mbona mwaka huu peke yake vijana zaidi ya 20,000 wamerudi majumbani kwao kwa sababu wamekosa mkopo wa elimu ya juu?
Wakati Rais anasema hayo nimejionea jana wafanyakazi wa TAZARA wakianza mgomo kwa sababu hawajalipwa mishahara ya miezi mitano, wakati huohuo nimeona walimu Kinondoni wakiandamana kudai fedha zao.
Badala ya kuanza kufikiri kipropaganda dhana ya kusomesha sekondari bure mwaka kesho, kwa nini tusilipe ada za watoto hawa masikini wa vyuo vikuu ambao wanahitaji msaada sasa hivi ili hayo ya mwaka kesho tuyapange wakati wa kampeni mwezi oktoba 2015?
Vyama vya upinzani viliposema utoaji wa elimu bure mwaka 2000, 2005 na 2010, CCM ilisema vinaongopa na haiwezekani na wananchi waliamini uongo wa CCM.
Hata hiyo elimu ya msingi tu CCM imeshindwa kutoa bure, michango iliyopo sasa inazidi ada ya zamani. Kinachoonekana hapo ni propaganda za kuanza kuwaweka sawa wananchi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka.
Si ajabu kuwa, Kinana na Nape watazunguka nchi nzima katika mikutano yao ya mwaka huu, wakieleza sera hii ya elimu ya sekondari ambayo kuitekeleza hawawezi.
Na hapohapo wanasahau kuwa mambo mengi yaliyoahidiwa na CCM mwaka 2010 hayajatekelezwa, Mahakama ya kadhi siioni, waliahidi!
Ni jambo la ajabu mno kukuta kiongozi wa nchi ambaye anamaliza muda wake anaanza kupanga ahadi za serikali ijayo, wakati uongozi wake umeacha majanga mengi katika nchi huku ukishindwa kutekeleza ahadi zake nyingi! Sijui mnanielewa?
J. Mtatiro,
Dar Es Salaam,
11 Januari 2015About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.