Thursday, January 8, 2015

KUTOKA IKULU YA DAR ES SALAAM LEO

unnamed
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha wajumbe sita wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Walioapishwa leo ni pamoja na mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Bahame Tom Mukiria Nyanduga,Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Iddi Ramadhani Mapuri, na makamishna wa Tume hiyo Bwana Mohamed Khamis Hamad, Dkt. Kevin Mandopi, Bibi Rehema Msabila Ntimizi, na Bibi Salma Ali Hassan.

                                                             

 Pichani Rais Kikwete akiwa pamoja na wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora aliowaapisha leo Watatu Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Bahame Tom Mukiria Nyanduga, Watano Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Iddi Ramadhani Mapuri, na makamishna wa tume hiyo wakwanza kushoto ni Bibi Salma Ali Hassan, Wapili kushoto ni Bwana Mohamed Khamis Hamad, Wasita kushoto ni Dkt.Kevin Mandopi, na kulia ni Bibi Rehema Msabila Ntimizi(picha na Freddy Maro).

   RAIS KIKWETE AMWAPISHA MSAJILI WA MAHAKAMA YA RUFAA

unnamed
unnamed1Msajili wa Mahakama ya Rufaa Bibi Katarina Tengia Revocati akipokea vitendea kazi kutoka kwa  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kula kiapo  ikulu jijini Dar es Salaam leo(Picha na Freddy Maro)

No comments: