Friday, February 13, 2015

LHRC YAWAPIGA MSASA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC leo kimeendesha mafunzo maalumu kwa waandhshi wa habari kadhaa nchini ambao wanahusika sana katika kuandika maswala ya haki za binadamu, mafunzo yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi katika Nyanja ya uandishi wa habari kuhusu haki za binadamu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa waandishi wa habari nchini ni nguzo muhimu sana katika kusimamia na kutetea haki za binadamu nchini hivyo mafunzo hayo yatawasaidia si tu waandishi bali pia wananchi ambao watakwenda kusaidiwa na waandishi hao.

Amesema kuwa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeeandaa mafunzo hayo kama njia moja wapo ya kuonyesha ushirikiano na wanahabari katika kutetea haki za binadamu kwani bila ushirikiano katika maswala ya haki za binadamu bado kutakuwa na matatizo.

Mkurygenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi HALLEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari hao wakati akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika jijini Dar es salaam leo
 Ameongeza kuwa bado nchini Tanzania kumekuwa na matatizo mengi ambayo yamekuwa yakiwakumba wananchi yakiwemo uonevu kutoka katika vyombo vya dola na sehemu nyingine ambayo yameku yakiwanyima wananchi haki zao za msingi hivyo akawataka waandishi wa habari kutumia mafunzo hayo kujiingiza katika kuwasaidia wananchi katika kupata haki za msingi.
Mtangazai wa radio free africa na star tv THOM CHILALA akisikiliza kwa makini katika semina hiyo iliyoandaliwa na LHRC leo jijini Dar es salaam
EMELDA URIO mmoja Kati ya wawezeshaji wa leo katika semina hiyo akizungumza
 Aidha bi HELLEN amewaasa wanahabari wa Tanzania kuacha mara moja tabia ya kutumika na watu kwa kupewa pesa ama aina yoyote ya rushwa ili kuficha madhambi Fulani ambapo amesma kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi na maadili ya uandhishi wa habari.

Katika mafuzo hayo ambayo yameendeshwa kwa siku moja na kuhudhuriwa na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini mada mbalimbali zimewasilishwa mezani na kujadiliwa kwa pamoja .

Baadhi ya mada ambazo ziliwasilishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na swala la katiba pendekezwa pamoja na mchakato mzima wa kupatikana kwake ambapo baadhi ya wanahabari na waliokuwa wanaendesha mjadala huo wameeleza wasiwasi wao mkubwa juu ya mchakato huo wa kuipata katiba mpya kwa kile walichodai kuwa umejawa na makosa mengi  na hivyo utapelekea kupatikana kwa katiba mbovu.

 Aidha mada nyingine iliyowasilishwa ni sheria ya kura ya maoni ambayo nayo pia imeeleezwa kuwa na vifungu ambavyo vinaashiria wazi kuwa vitaleta vikwazo vikubwa katika mchakato wa kupata katiba mpya.

Baadhi ya wanahabari waliopata nafasi ya kuzunguma na mtandao huu wamekiri kuwa mafunzo haya yamewafungua macho kwa kiasi kikubwa na yatawasaidia sana katika utendaji wao wa kazi .

KWA PICHA NYINGINE ZA MAFUNZO HAYO ZIPO CHINI










No comments: