Mwenyekiti wa mtandao huo Ms MARTINA KABISAMA (katikati) akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam |
Mtandao wa asasi za
kiraia wa kuangalia chaguzi Tanzania (TACCEO) umeitaka serikali kutimiza wajibu
wake wa kuipatia fedha za kutosha tume ya taifa ya uchaguzi ili kutimiza wajibu
wake kwa wakati kutokana na kuonekana tume hiyo kusua sua katika zoezi la uandikishwaji
wa daftari la kudumu kunakotokana na kukosa fedha za kutosha kuendesha zoezi
hilo.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dare s salaam na mwenyekiti wa mtandao huo Ms MARTINA KABISAMA wakati
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu zoezi la uandikishwaji wa wapiga
kura kwa mfumo wa kielektronic BVR ambao mtandao huo umekuwa ukifanya uangalizi
katika mikoa ambayo tume inaendesha zoezi hilo.
HAMIS MKINDI ambaye ni mratibu wa TACCEO akizungumza mbele ya wanahabari leo |
Amesema kuwa ni wazi
kuwa zoezi hilo limekuwa likienda taratibu kutokana na sababu kubwa za tume
kutokuwezeshwa kikamilifu kwa fedha za kuendesha zoezi hilo jambo ambalo
limekuwa likikwamisha zoezi hilo katika maeneo ambayo wamefanya uandikishwaji.
Katika uangalizi wa
mikoa ya Njombe,Lindi,Mtwara, na Ruvuma wamesema kuwa timu ya waangalizi kutoka
mtandao huo wameweza kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria,na kanuni za uchaguzi
pamoja na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi huku akisema kuwa endapo
mapungufu hayo hayatafanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo itapelekea wananchi
kupoteza haki yao ya msingi ya kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi kwa
mujibu wa sheria.
Akitaja baadhi za
changamoto za ukiukwaji wa sheria zilizotokea katika mikoa ambayo zoezi hilo
linaendelea Ms KABISAMA amesema
kuwa,kutokutolewa kwa elimu ya mpiga kura vijijini, wananchi kuandikishwa bila
alama za vidole, uandikishwaji kufanya hadi saa sita usiku,pamoja na vituo vya uandikishwaji
kuwekwa katika nyumba za ibada,hospitali na kwenye mabanda ya mama lishe ni
moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza katika zoezi hilo.
Nyingine ni uandikishwaji
kushindwa kufanyika kwa wakati kutokana na kukosekana kwa mashine za kuandikishwa
na kuishiwa kwa chaji,wananchi wengi kuachwa kuandikishwa kutokana na
kumalizika kwa siku saba zilizopangwa kwa ajili ya maeneo hayo, nazo zimekuwa
sababu ambazo amezitaja kama zinaweza kukwamisha wananchi kushiriki kikamilifu
katika zoezi hilo.
Aidha amesema kuwa kutokana
na kasoro hizo zilizojitokeza (TACCEO) wamaitaka tume ya Taifa ya uchaguzi
ihakikishe kuwa inarekebisha kasoro hizo ikiwa ni pamoja na kurudia maeneo
ambayo wananchi walikosa haki hiyo ya kujiandikisha kwani ni haki yao ya msingi,huku
akiitaka tume hiyo kuruhusu asasi za kiraia kutoa elimu ya uraia kwa wananchi
ili kuweza kuhamasisha kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo.
Mtandao wa asasi za
kiraia wa kuangalia chaguzi Tanzania TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na
haki za binadamu LHRC umekuwa ukishiriki uangalizi wa zoezi la uandikishwaji
wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektronic BVR ulioanza rasmi tarehe
23,mwezi wa pili 2015 katika halmashauri ya mji wa makambako
No comments:
Post a Comment