Tuesday, May 19, 2015

TANZANIA KWENYE USHINDI MWINGINE,IRENE KIWIA ASHINDA TUZO YA MWANAMKE BORA AFRICA

 Jukwaa la wanawake ambao wameleta michango mikubwa nay a ajabu ya ukuaji wa maendeleo ya mataifa mbalimbali barani Africa (AFRICAN-RECONECT) wametoa tuzo kwa waafrica 11 ambao wamefanya vizuri na kuleta michango ya uwezeshaji katika bara la Africa.

Katika sherehe za tuzo hizo ambazo zilifanyika nchini Africa ya kusini zilishughudia mwanaharakati wa maswala ya maendeleo ya wanawake mwanadada IRENE KIWIA akinyakua tuzo ya mwanamke bora wa Africa katika watu 11 walionyakua tuzo hizo huko Africa ya kusini.
Akizngumza mara baada ya kutajwa kuwa mshindi wa nafasi ya mwanamke bora barani Africa IRENE KIWIA amesema kuwa barani Africa kuna wanawake wengi ambao wanafanya mambo makubwa na ya ajabu lakini anashukuru kwa heshima kubwa aliyopewa na jukwaa hilo ya kuonekana yeye ndiye anayestahili kupewa tuzo hiyo na kuwa mwanamke bora barani Africa.

Amesema kuwa tuzo aliyoipata ni maalumu kwa wanawake wote ambao wanafanya mambo si kwa ajili yao wenyewe tu bali wanafanya kuhakikisha watu wengine wananufaika,wanawake ambao wanaamini kuwa kufanya vizuri ni lazima kwanza ufanye mambo mema,wanawake ambao hutenda mambo mema k3wa watu bila mkujali wao watanifaika nini,na wanawake wote barani Africa ambao wakiamka hufikiri na kupanga mambo juu ya watu wengine.

Amesongeza kuwa wanawake wa Africa mungu amewapa uwezo mkubwa na wakipee wa kulea kitu chochote,hivyo kumuheshimu mwanamke wa Africa na kutambua uwezo wake ni jambo muhimu kwa ukuaji wa bara la Africa.

Amesema kuwa bara la Africa litakuwa kikamilifu pale ambapo tu mwanamke ataondokana na umaskini,atapata elimu bora,afya bora,pamoja na pale ambapo mwananke wa Africa atakuwa ni kitovu cha uchumi wa bara lake.
Amesema kuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya juu ya wanawake lengo lake ni kuboresha maisha ya mwanamke,kupanua fursa,na kuwasaidia wanawake wa Tanzania  ambao nao wataisaidia jamii ambayo inawazunguka,huku akisema kuwa ni lazima waafrica tuungane kwa pamoja kuwasaidia wanawake ambao wameshindwa kufikia malengo yao wa weze kuyafikia.


Akizungumza mara baada ya utoaji wa tuzo hizo mwanzilishi wa African reconnect Bi CHENGETA amesema kuwa ni furaha kuona wanawake ambao wamefanya mambo makubwa wakitambuliwa mchango wao kwani itasaisaidia kuamsha hari na motisha kwa wanawake wengine barani Africa kufanya mambo makubwa zaidi kwa mataifa yao.
African-reconect ni jukwaa la wanawake ambao wamefanya mambo makubwa nay a ajabu kwa ukuaji wa mataifa mbalimbali barani Africa.

No comments: