Tuesday, June 16, 2015

BREAKING NEWZZ--VIKUNDI VYA ULINZI WA VYAMA VYAPIGWA STOP MUDA HUU,SOMA HII

Kikundi cha CHADEMA cha REDBRIDGED 

 Dakika chache zilizopita habari kutoka katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ni kuwa msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji MUTUNGI ametangaza kupiga marufuku vyama ambavyo vinamiliki vikundi mbalimbali vya ulinzi na usalama kwa kusingizia kuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa vyama hivyo na kuvitaka kuvifuta mara moja kwani ni kinyume na sheria za Tanzania kwa chama kumiliki kikundi ambacho kinapewa mafunzo ya aina yoyote ya kijeshi.

Kikundi cha ccm cha GREENGUARD
Amesema kuwa sheria za Tanzania pamoja na katiba zinapiga marufuku kwa chama chochote cha siasa kiwe kimesajiliwa au hakijasajiliwa kumiliki kikundi ambacho kitakuwa kinafanya kazi sawa na jeshi la polisi au majeshi ya Tanzania ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo jukumu la kulinda raia na mali zao linabaki kuwa la jeshi la polisi Tanzania.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Amesema kuwa vikundi hivi vilianzishwa wakati wa mfumo wa chama kimoja na vilikuwa ni vikundi vya wanachama waliopewa jukumu la kuangalia ulinzi wa mali za chama husika,kulinda viongozi na kupanga wanachama wakati wa mikutano ya kisiasa ambapo amesema kuwa kipindi hicho wanachama hao walikuwa kama wanafamilia na hawakuwa wakipewa mafunzo ya aina yoyote ya kijeshi kama inavyoonekana sasa katika vyama kadhaa nchini Tanzania.


Aidha amesema kuwa baada ya mfumo wa vyama vyingi vya siasa kuingia nchini Tanzania sheria hiyo haikubadilika na badala yake waliamini kuwa vyama hivyo vingefwata shertia zilizowekwa na nchi lakini badala yake imeonekana kukiuka sheria hizo.

Baadhi ya vyama ambavyo vinamiliki vikundi hivyo ni pamoja na ccm ambao wanakikundi cha greenguard,chadema na kikundi cha Redbridged,pamoja na chama cha wananchi cuf na kukundi cha blueguard.


No comments: