Tuesday, June 30, 2015

GHASIA:HALMASHAURI ZIACHE KUTEGEMEA SERIKALI KUU

Baadhi ya Halmashauri manispaa zimeonywa kuwa na tabia ya kuitegemea serikali kuu na badala yake iwe na vyanzo vya mapato vya ndani kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo katika halmashauri zake.

Hayo yalielezwa na Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia wakati wa kufungua kongamano la  utekelezaji wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 lililofanyika mkoani Mtwara iliyokuwa na kuuli mbiu isemayo, “Mwananchi pigia kura katiba pendekezwa na chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.

Ghasia alisema kuwa halmashauri nyingi zimekuwa tegemezi  na hivyo pale pesa zinapochelewa kufika katika maeneo yao zimekuwa zikishindwa kusonga mbele zaidi katika miradi na hali hiyo inasababishwa na kukosa vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri.

“Kazi ya serikali kuu ni kutunga sera na kusimamia pamoja na kuweka viwango, lakini ikumbukwe serikali za mitaa kazi yake ni kutekeleza kwani zipo karibu na wananchi kwahiyo mwanachi wa kawaida akilalamika moja kwa moja analalamnikia mamlaka za serikali za mitaa,”alisema Ghasia
Akizungumza Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Didas Masaburi alisema kuwa asilimia kubwa halmashauri nyingi zinakumbwa na madeni kutokana na kukosa vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri kutokana na kuitegemea serikali kuu.

Alisema hakuna halmashauri hata moja ambayo haina deni chini ya miaka miwili ama mitatu kutakana na mapato wanayopata kutoka serikali kuu kuweza kuchelewa ama kuwa madogo na hivyo kushindwa kujiendeleza.

“ Tatizo la halmashauri kutegemea serikali kuu bado ni changamoto kubwa sana kwani wengi wao hawana vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri na ukiangalia halmashauri zote hakuna hata moja ambayo haina deni si la chini ya miaka miwiliama mitatu,”alisema Masaburi na kuongeza
“ Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi wameshafungua jicho wanaona halmashauri zinaweza kujiendesha na sisi tunaona hivyo kwa hiyo halmashauri zisipoweza kujikwamua na serikali kuu itakaleta pesa itafikia mahali halmashauri zikashindwa kujiendeleza ama zikafa ni lazima ifikie wakati tujirekebishe kwasababu madeni ni makubwa na pesa hazitoshi kawani halmashauri nyingi zinaanza kufanya mambo mapya na kuacha yale ya zamani,”alisema Masaburi

Akizungumza mmoja wa washiriki, mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Ally Mtopa alisema kuwa makusanyo katika halmashauri kama yakisimamiwa vizuri yanaweza kusaidia kupunguza utegemezi toka serikali kuu na kuicha miradi mikubwa kuungwa mkoano na serikali kuu.

Hata hivyo alisema kuwa endapo serikali kuu itachelewa kupeleka fedha ama kutopeleka kabisa kuna hatari ya kuzipelekea halmashauri za miji na manispaa nchini kufa
“Makusanyo yakiwa vizuri ndani ya halmashauri yanaweza kusaidia kupunguza kutegemea bajeti toka halmashauri kuu na hivyo ile miradi mikubwa itabidi serikali kuu ituunge mkono tofauti na hapo itabidi tusubiri kila kitu toka makao makuu na kama wakichelewesha ama kutoleta kabisa halmashauri za miji na manispaa zinaweza kufa,”alisema Mtopa

No comments: