Tuesday, June 16, 2015

SIKU YA MTOTO WA AFRICA-WATOTO WALIA NA SERIKALI

Mtoto ANTHONIA SANGEDA kutoka shule ya ST MARRY MAZINDE JUU akizungumza na wanahabari wakati wakisoma tamko lao juu ya siku ya mtoto wa Africa na changamoto zinazowakabili wao kama watoto
 Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya Mtoto katika bara la Africa serikali ya Tanzania imetakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa haki ya motto wa kitanzania inatambulika na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoto wanatambulika katika katiba na sheria mbalimbali ili kuwasaidia kuypata haki zao za msingi.

Wito huo umetolewa na watoto mbalimbali waliopo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa afica ambayo wanayafanyia kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wakati wakitoa tamko kwa vyombo vya habari kuhusu siku ya mtoto wa Africa.
Wamesema kuwa wanaamini ikiwa serikali itaamua kwa dhati kuweka mfumo mzuri ambao utamuwezesha mtoto kuwa katika mazingira salama itakuwa ni hatua mbadala ya kumlinda mtoto wa kitanzania ikiwa ni pamoja na kuwepo mfumo imara  wa mawasiliano ambao utamwezesha mtoto kufikisha maoni yake katika ngazi husika pale ambapo atakuwa anakosa haki zake za msingi.

Mtoto CHANDE MOHAMED  kutoka shule ya PENDAMOYO Jijini DAR ES SALAAM akizngumza na wanahabari
Katika tamko hilo limeanisha mambo mbalimbali ambayo bado ni changamoto kwa watoto wa kitanzania huku kubwa likiwa ni tatizo la mimba za utotoni ambalo kwa kipindi cha hivi karibuni limeshika kasi sana na kuleta madhara makubwa kwa watoto wengi ikiwa ni pamoja na kuwaharibia ndoto zao za kimaisha.
Wameeleza kuwa matatizo hayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisababishwa na kutokuwepo kwa mfumo inara wa ulinzi kwa mtoto hasa kwa watoto wa kike,kutokuwepo kwa mfumo wa utoaji elimu kwa jamii ya watanzania juu ya haki za mtoto,pamoja na kutokuhukumiwa kwa watuhumiwa wanaokiuka sheria za haki ya mtoto.
Wanafunzi mbalimbali waliohudhuria kuadhimisha siku ya mtoto wa Africa makao makuu ya kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC
Wamesema kuwa kutokana na hayo mtoto wa kitanzania ameendelea kuwa chini huku akikosa haki zake za msingi huku wizara husika na taasisi husika kushindwa kuwajibika ipasavyo kuhakikisha mtoto anapata haki zake kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELLEN KIJO BISIMBA akizungumzia siku hiyo ya mtoto wa Africa
Aidha watoto hao wameishauri serikali kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya haki za mtoto kwa umma jam,bo ambalo wamesema kuwa litasaidia katika kukuza uelewa wa jamii kuhusu haki za mtoto wa kitanzania.

No comments: