.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MUFTI SIMBA, ASHIRIKI KISOMO

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha marehemu Simba. Picha na OMR

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha marehemu Simba. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata, Kinondoni kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha Marehemu Simba, leo Juni 16, 2015. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi katika Kisomo cha kumuombea Marehemu Mufti Shaaban Bin Simba, kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweny Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo inondoni, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa Kisomo cha kumuombea marehemu Bin Simba, kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweye Viwanja vya Ofisi za Bakwata Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki swala maalumu ya kuswalia Jeneza (halipo pichani) na baadhi ya viongozi wa kitaifa wakati wa kisomo maalumu kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuombea marehemu. Picha na OMR

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.