Saturday, June 20, 2015

TIZAMA MEMBE ALIVYOTUA BUKOBA IKAWA HIVI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Kagera mjini Bukoba Juni 20.2015, alipokwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mbele mwenye miwani) akiongoza umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera Juni 20.2015 na kufanya matembezi kutoka uwanjani hapo hadi katika Ofisi ya CCM Mkoa, alipokwenda kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo. Kushoto kwake Ini Katibu mstaafu wa CCM mkoa Kagera, Faustine Kamaleki.

Msafara wa bodaboda ukiongozi msafara wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (hayupo pichani) baada ya kuwasili mjini Bukoba mkoani Kagera Juni 20.2015,kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo.

No comments: