Sunday, June 14, 2015

WAZIRI BERNARD MEMBE APATA UDHAMINI ZANZIBAR

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akilakiwa na  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Mjini Unguja, baada ya kuwasili kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Aman kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akifurahia jambo pamoja na  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Mjini Unguja, kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Aman jana waliofika kumdhamini ili awanie Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kati, Ally Yusuf Salim zilizojazwa na wanachama wa CCM mkoa wa Kusini Unguja jana kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja. Kushoto ni Katibu wa CCM Kata ya Jumbi, Christina Athony.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akishuhudia mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitia saini kumdhamini kwenye fomu yake ya kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, katika ofisi ya CCM wilaya ya Kaskazini ‘B mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar jana, ambapo alipata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote mine ya Unguja. Katikati ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM  wilaya hiyo, Haji Machano Haji. Picha zote na John Badi

No comments: