Wednesday, July 1, 2015

TIZAMA HISTORIA MPYA WALIYOWEKA SIMBA SC LEO

Afisa MtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu Wakiwa wameshika Mfano wa Kadi ya Club Hiyo waliyoizindua Leo.
Klabu ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama ambazo zinamwezesha kila Mwanachama wa Simba kupata bima ya maisha hadi Tsh 250,000 ikiwa atafiwa na mwenza au mtoto au yeye mwenyewe kupitia bima ya maisha iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba leo hii imezindua Kadi za watoto yaani Simba Cubs.
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akimkabidhi Mtoto Iqram Ally Kadi ya Simba Cubs waliyoizindua leo wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (kulia) Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange.
Akizungumza wakati wa uzinduzi Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendajii kifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita hapa kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.(VICTOR)
Aliongeza kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz . Napenda mtambue hii ni historia katika ukanda huu kuweza kutumia teknojia kufikia wanachama, Sisi ni wakisa sana tunaona mbele!.
AfisaMtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (Kulia) Akielezea Jambo Akiwa Ameambatana na Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Wakati wa Uzinduzi wa Kadi Hiyo ya Simba Sport Club Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati ya masoko na biashara Imani Kajula alisema
‘’ Uanzishwaji wa Kadi ya Simba Cubs itawawezesha watoto sio tukutambuliwa kuwamemba wa Simba, bali pia kupata punguzo kubwa au kuingia bure kwenye matukio yanayo andaliwa na Simba Sports Club. Pia maduka mbalimbali yatatoa punguzo kwa watoto wenye Simba Cub Card.
Wote mna jua fika kuwa mapenzi hujengwa, Simba ina lengo la kujenga msingi imara wa kuendeleza wanachama na wapenzi wake’’.

No comments: