Kampuni ya
uchimbaji mafuta na gesi ya Swala Energy leo imetimiza mwaka mmoja tangu
kuingia katika soko la hisa (IPO) huku ikiahidi makubwa katika sekta hiyo.
Swala Energy ni
kampuni ya kwanza ya uchimbaji nishati hizo kuingia katika soko la hisa la Dar
es Salaam (DSE) na kuwapa nafasi Watanzania kuweza kununua hisa na kuwa
wamiliki wa kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi Mkuu wa Swala Energy Bw. David Mestres Ridge, Swala
Energy ambayo hivi karibuni iliuza asilimia 25 ya hisa zake kwa kampuni ya Tata
Petrodyne Ltd, mbali ya hilo mwanzoni mwa mwezi August kampuni ya Swala ilipewa
kibali na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ili kuvuna asilimia 50
ya mapato katika leseni zake za Kilosa na Pangani.
Kwa mujibu wa Bw. Ridge,
kinachosubiriwa kwa sasa ni ruhusa kutoka Tume ya Ushindani isiyofungamana na
upande wowote (FCC) ili kuanza utekelezaji huo, “tuna imani ya kwamba ridhaa
kutoka FCC itakuja hivi karibuni ili tuanze utekelezaji wa mipango yetu.”
Chini ya makubaliano haya, TPL
itazalisha kwa niaba ya Swala ambapo mikakati yote itakuwa tayari kutekelezwa,
“ninawashukuru sana Wizara ya Nishati na Madini kwa kuturuhusu kufanya utafiti
na kuchimba nishati hizi, tunaahidi kuwafanyia Watanzania makubwa zaidi pindi
tukianza uchimbaji.”
No comments:
Post a Comment