Wakati Umoja wa Katiba
ya wananchi UKAWA ukikumbwa na changamoto ya ugawanaji wa majimbo baada ya
maeneo mengi nchini Tanzania kuibuka migogoro mara baada ya majimbo ya uchaguzi
kugawanywa kwa vyama hivyo,hatimaye mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI ambaye
ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo ameibuka na kutoa onyo kali kwa viongozi
ambao wanakuwa wabinafsi wa kutokutaka kuachiana majimbo na kusema kuwa
ubinafsi ni jambo ambalo halitaendekezwa ndani ya umoja huo.
Akizungumza na
wanahabari leo jioni hii Dar es salaam amesema kuwa mara baada ya kukamilika
kwa kazi ya kugawana majimbo kwa vyama vinne vinavyounda umoja huo kumeibuka
sintofahamu ya baadhi ya watu kungangania majimbo ambayo tayari wamepewa watu
wengine jambo ambalo amesema kuwa sio makubaliano ya umoja huo na hawatavumilia
viongozi wa namna hiyo.
Amesema kuwa moja ya
maazimio makubwa ya umoja huo ni kuepuka ubinafsi na kuhakikishya kuwa mambo
wanayoyahubiri kwa wananchi wanayatekeleza kwa vitendo ikiwa ni pamoja na amani
na umoja hivyo hawako tayari kuona chama au mtu yoyote anaanzisha vurugu ndani
ya umoja huo.
Amesema Tayari leo
jioni viongozi wakuu watakutana kuona ni jinsi gani wanaweza kushughulikia
jambo hilo ili ndoto za watanzania za kuhakikisha kuwa wanauondoa mfumo dhalimu
wa CCM uliopo kwa sasa zinatimia na nchi inakuwa na amani na utulivu mkubwa.
KUHUSU STORY YA CHAMA
CHAKE KUJITOA UKAWA
Akizngumzia sakata hilo
ameonyeshwa kushangazwa na taarifa hizo huku akisema kuwa atakuwa ni kichaa kama
mtu aliyeasisi mageuzi nchini Tanzania anaweza kuyakimbia kipindi ambacho
mageuzi yanazaa matunda mazuri.
Amesema kuwa UKAWA ni
zao la NCCR mageuzi kwa kuwa lengo kuu la ukawa sasa ni kufanya mageuzi ya
mfumo uliopo sasa na kuweka mfumo ambao ni rafiki kwa wananchi hivyo hana
mpango na hawezi hata siku moja kujitoa katika umoja huo na story zinazoenea ni
muendelezo wa mbinu chafu za wapinzani za kujaribu kuwagombanisha ndani ya umoja
huo jambo ambalo amesema wamechelewa
kulifanya.
KUHUSU KUPIGWA MARUFUKU
KUTUMIA UWANJA WA TAIFA KUZINDUA KAMPENI.
Mbatia akizungumza kwa mshangao mkubwa amesema kuwa hajaona sababu ya msingi na
ya uhakika ya kuzuiliwa kufanya shughuli zake ndani ya uwanja wa taifa ambao
ulijengwa na kodi ya watanzania huku akisema kuwa yote hii ni kutokana na
serikali kumaliza sehemu zote za wazi kwa kuwauzia watu na sasa watanzania hawana
hata mahali pa kukutana na kujadili mambo yao wakiwa na amani.
Pamoja na katazo hilo
la serikali MBATIA amesema kuwa haliwezi kuwazuia kukutana na watanzania hivyo
leo jioni watajadili kwa pamoja na kupata majibu kuwa ni wapi na lini wanaweza
kuzindua kampeni zao kwa kumnadi mgombea wake wa nafasi ya urais
No comments:
Post a Comment