Friday, August 7, 2015

NEWZZ...UKAWA sasa ni vyama 6,hivi vyama viwili vimejiunga leo


Wakati vyama vinne vinavyounda UKAWA, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyama vingine vya SAU na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. 

Katibu Mkuu wa SAU, Ali Kaniki alisema chama hicho kimefikia uamuzi wa kuunga mkono umoja huo kutokana na nafasi kubwa iliyopo ya kushika dola. Kaniki alisema kwa sasa wana wanachama zaidi ya 500,000 nchi nzima, hivyo wanaamini kuwa na mchango katika harakati hizo. 

Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema chama hicho kinaamini mabadiliko kupitia kambi ya upinzani, hivyo wameamua kuunga mkono UKAWA. 

“Uchaguzi wa mwaka 2010, nilishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,000, lakini pia tuna madiwani watatu na wanachama wameongezeka kwa hivyo ninaamini mchango wetu utakuwa na nafasi kubwa UKAWA,” 
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam, Joackim Mwakitinga alisema chama hicho kitakuwa tayari kuunga mkono mgombea mmoja kutoka CCM au UKAWA.
“Nafasi ya urais hatutasimamisha mgombea ila tutaunga mkono kati ya vyama hivyo wakati wa kampeni.”

No comments: