Sunday, September 13, 2015

Video---Mnyika amtaka Waziri MEMBE aache kuwatisha waangalizi wa Uchaguzi





Baada ya waziri wa mambo ya nje Bernad Membe kuwapa tahadhari waangalizi wa uchaguzi kutoka nje ya Tanzania kwa kuwataka kuwa makini na taarifa watakazokuwa wanazitoa naye naibu katibu mkuu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA MHh JOHN MNYIKAameibuka na kupinga kauli hiyo huku akisema kuwa hivyo  vitisho na kamwe waangalizi hao wazitishwe na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi yao

Mapema wiki jana Akizungumza na mabalozi kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba mwaka huu, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe aliwataka waangalizi wa kimataifa kutofungamana na upande wowote ambapo amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya kutoa taarifa na kusisitiza iwapo watabaini mapungufu yoyote wanapaswa kupeleka kwa tume ya uchaguzi baada ya tume kutoa taarifa

Kauli hiyo mnyika anasema ni mbinu za kuwapunguza nguvu waangalizi hao na kuwafanya washindwe kupinga magoli ya mkono yatakayokuwa yanafungwa na chama cha mapinduzi katika uchaguzi huo..
Habari24 tv imekuletea kauli za John mnyika tizama video hapo chini

No comments: