Wednesday, September 30, 2015

VIDEO--Sheikh HEMED JALALA asimulia mkasa mzima aliyoyaona kwenye ibada ya HIJJA


Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA ameibebesha mzigo wa lawama serikali ya Saudi Arabia kufwatia vifo vya watu zaidi ya elfu nne vilivyotokea siku chache zilizopita wakati wa Ibada ya hija iliyofanyika nchini humo huku akisema kuwa vifo hivyo ni uzembe wa wazi wa waandaaji wa ibada hiyo.

Lawama hizo amezitoa leo Jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili nchini Tanzania pamoja na waumini wengine wa dhehebu hilo wakitokea katika ibada hiyo ambapo amesema kuwa ni wazi mauaji yaliyotokea katika ibada hiyo ni ya kusikitisha sana na yalitokana na uzembe wa waandaaji wa ibada hiyo kutokana na kasoro nyingi zilizoonekana.

Amesema kuwa moja ya sababu kubwa iliyosababisha mauaji ya waumini wengi ni kufungwa kwa njia kubwa za kutoka na kuingilia wakati wa urushwaji wa mawe kumpiga shetani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa wa watu na kusababisha vifo vingi.

Aidha Sheikh JALALA ameongeza kuwa katika maeneo yote ya ibada hiyo kulikuwa kumezungukwa na kamera eneo lote lakini watu walikuwa wakifariki kwa mfululizo kwa kila baada ya dakika tatu lakini wahusika hawakuona na hakuna msaada wowote ambao ulikuwa unatolewa na wahusika licha ya kuwepo kwa kamera kila kona.

Baada ya tukio hilo Sheik jalala amesema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa ni lazima serikali ya Tanzania iungane na nchi ambazo zina idadi kubwa ya mahujaji ambao wanaenda katika ibada hiyo waweze kushirikishwa katika mipango ya ibada hiyo ili kuweka mipango ambayo itawafanya waumini kuwa salama wakati wa ibada hiyo kwa kuwa hakuna mtu anayekwenda katika ibada hiyo kwa ajili ya kufa.

No comments: