Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
KATIKA hali inayoonyesha ni joto kali la kuwatumikia Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, amepiga marufuku likizo za Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
RC Makalla aliyasema hayo juzi katika kikao cha kazi na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara wa halmashauri na Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa huo kwa ajili ya kupeana mikakati ya majukumu ya kuwatumikia Wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni hatua nzuri ya kwenda na kasi ya Dr Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa huo ili kujipanga katika majukumu mbalimbali ya kuwatumikia wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Baadhi ya watendaji wa Mkoa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo, Aamos Makalla alipozungumza nao jana. Katika kikao hicho, RC Makalla alipiga marufuku likizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara ili kujipanga na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.