Thursday, November 19, 2015

LIPUMBA AJIUNGA TENA UKAWA KIAINA,SOMA ALICHOWAAMBIA WANAHABARI LEO

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba ameibuka tena,na sahivi amemtaka Rais John Magufuli kuiamuru Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kumtangaza Mgombea wa Urais kupitia CUF,Maalim Sef sharif Hamadi kuwa mshindi wa Nafasi ya Urais.
        Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho , miezi mine iliyopita kutokana na kutoelewana  na Viongozi wa vyama vya UKAWA 


   LIPUMBA leo ameibuka  kwenye makao makuu ya Ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni jijini hapa na kuzungumza na waandishi wa habari  na kuzungumzia mgogoro mkubwa unaoendelea visiwani Zanzibar na kusema hali hiyo ikiendelea hivyo itaweza hata kuvuruga umoja ambao Taifa unao na kupelekea kukwamisha shuguli zote za kimaendeleo.

    “Namuomba Rais Magufuli aliokoe Taifa lilipofikia kwa kuiamuru ZEC kutangaza matokeo ya Urais yaliyobakia lasivyo,kama naye akiendelea kuacha uvunjifu wa Katiba ya Zanzibar basi Taifa halitaweza kusonga mbele litakuwa kila siku lipo kwenye mgogoro”

      Amesema kitendo cha Rais Magufuli kwenda kulihutubia Bunge kesho na kuongozana na Rais wa  Zanzibar anayedai amemaliza mda wake Dk Mohamed Shein hakikubaliki na kinakwenda  kinyume na katiba ya Zanzibar.

     “Leo Magufuli najua ameaapa na kuilinda Katiba,itashangaza kuona Kesho Dk shein ataingia kwenye Bunge wakati ni ukweli kwamba katiba ya Zanzibar inaonyesha wazi ameshamaliza mda wake wa uongozi kwa kipindi cha miaka mitano,sasa kama kesho akiwepo kitendo hiko hakitakubalika na kinafaa kupingwa ka kila Mtanzania”amesema Profesa Lipumba.

      Kuibuka huko kwa Profesa Lipumba kunakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya Wabunge wanaounda muunganiko wa Vyama vya Ukawa,kumwandikia Barua Spika wa Bunge wa Job Ndugai na kutaka uhalali wa Rais Magufuli kuhutubia Bunge wakati Zanzibar bado hawajapata Rais wake.

      Akisoma Barua hiyo jana Mjini Dodoma kwa niaba ya Wenzake mwenyekiti mwenza wa Umoja huo,Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Ukawa hawatakakubali katika mazingira yeyote kuruhusu katiba ya nchi ambayo imetokana na matakwa ya wananchi ikuvunjwa hadharani.

     Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hai amesema njia pekee watakayotumia mwaka huu si ile waliyotumia mwaka 2010 kumsusia Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoka nje kuhu wakidai njia watakayoitumia sahivi ni kupambana ndani ya Bunge mpaka haki itakapopatikana.

      Huku wakificha njia watakayotumia kwa kuwataka wanahabari wasibuli siku hiyo ifike.

No comments: