Thursday, April 21, 2016

Tigo yatangaza Video za YouTube kupatikana bure usiku

Mkuu wa kitengo cha vifaa na mawasiliano wa Tigo DAVID ZAKARIA akitangaza kuanza kwa huduma hiyo mpya kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo ambapo sasa wataweza kupata kutizama video Bure kutoka YouTube kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili Alfajiri bure kabisa



 Kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania inayoongoza kwa huduma bora za kidigitali TIGO leo imetangaza upatikanaji wa huduma ya bure ya kutiririsha video za youTube nyakati za usiku kwa watumiaji wake wote ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa huduma hiyo kwenye mitandao ya kijamii  bila tozo hapa nchini.

Akitangaza ofa hiyo leo jijini Dar es salaam mkuu wa kitengo cha vifaa na mawasiliano wa Tigo DAVID ZAKARIA amewaeleza wanahabari kuwa huduma ya kutiririsha video za youTube bure itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa tigo kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri ambapo wateja wa Tigo Zaidi ya million kumi watanufaika na huduma hiyo.

Amesema kuwa kitu pekee kinachohitajika ili kuweza kupata huduma hiyo ni kuwa na aina ya simu yenye uwezo wa internent ambapo amezidi kusema kuwa huduma hiyo inazidi kuonyesha wazi jinsi gani mtandao wa Tigo umekuwa ukijituma kwa watumiaji wake ili kuwapa huduma bora Zaidi za kimtandao.
Meneja mawasiliano wa Tigo JOHN WANYANCHA akisisitiza jambo mbele ya wanahabari juu ya Huduma hiyo
Aidha pamoja na utiririshaji huo wa video youTube wateja watakuwa na njia mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni program ya simu inayojulikana kama youtube Offline inayomwezesha mtumiaji kuongeza video kwenye simu yake ili aweze kuiangalia baadae wakati ambapo muunganisho wa internent unakuwa haupo au upo chini.

Pamoja na hayo kwa video ambazo pale ambapo zinapatikana watumiaji wanaweza kuchagua kuongeza video kwa kuzitiririsha na kwa ajili ya kuangalia hapo baadae kwa kutumia kitufe cha offline ambapo ikiwa imeshachukuliwa kwa njia hiyo video hiyo inaweza kuchezesha bila kuunganishwa na internent kwa muda wa hadi saa 48 hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za youtube bila hofu ya muunganisho wa internent kuwa yapo chini.
Wanahabari mbalimbali wakiwa katika mkutano huo
Zakaria ameongeza kuwa kuzifikia data bure kutakuwa kunapatikana kwa wateja wa Tigo malipo kabla bila kuwepo malipo maalum yanayohitajika kuifurahia huduma hiyo.utiririshaji wa video za bure kutoka youTube umefanyika baada ya Mtandao huo kutangaza huduma nyingine za bure ambazo ni whatsapp kwa wateja wake ambapo pia ilitanguliwa na kuzinduliwa kwa huduma ya  Facebook ya kishwahili hapo mwaka 2014.

Mtandao wa YouTube ulizinduliwa mwaka 2005 ambapo unatumiwa na wafuasi Zaidi ya Billion moja duniani kote takribani theluthi moja yake wakiwa wanatumia internent.ambapo imekuwa ikiwapa nafasi wateja wake kutizama video mbalimbali,pamoja na kutoa maoni kuhusu video hizo.

No comments: