Thursday, June 2, 2016

YALIYOJIRI NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO MJINI DODOMA JUNI 2, 2016.


 Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto), Mhe.
Margaret Sitta Mbunge wa Urambo (katikati) na Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakielekea ndani ya Ukumbi
wa Bunge, Dodoma leo.


 Baadhi
ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Baadhi
ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha
kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
 Mchezaji
wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem
Thabeet (kulia) akiwa na  baadhi ya
wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge leo.
 Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akichangia jambo wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo.
 Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni akijibu maswali ya
wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.
 Baadhi
ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge
wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
 Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia)
akisalimiana na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa
Bunge leo mjini Dodoma.Katikati ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia)
akizungumza jambo na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga (kushoto) na Mbunge
wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Mchezaji
wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem
Thabeet (kushoto) akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (wa pili kutoka kushoto) na baadhi ya Wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Mwenyekiti
wa Kamati ya Haki , Maadili na Madaraka ya Bunge na Mbunge wa Newala Mhe.
George Mkuchika (katikati) akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe.
Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
 Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsisitiza jambo Meneja wa VETA mkoa wa Iringa  Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.
 Kiongozi
wa Kambi ya Upinzania Bungeni Mhe. Freeman Mbowe akifurahia jambo na Mbunge wa
Mtera Mhe. Livingstone Lusinde nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
 Wabunge
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), ,
Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mhe. Joseph Kasheku Msukuma
( pili kutoka kushoto)wakifurahia jambo
na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya
Ukumbi wa Bunge leo.
 Mbunge
wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), Mbunge wa Mtera Mhe.
Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mbunge wa Geita vijijini Mhe.
Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakimweleza jambo Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni leo mjini Dodoma.
Picha
na Aron Msigwa na Fatma Salum–MAELEZO, DODOMA.

No comments: