Tuesday, August 16, 2016

Hiki ni chama kingine kilichoibuka kupingana na UKUTA wa CHADEMA


Na Maelezo-Zanzibar
Chama cha Wakulima (AFP) kimelaani vikali dhidi ya hujuma zilizoandaliwa kufaywa na Umoja wa Wananchi UKAWA ifikapo tarehe 1mwezi ujao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Chama hicho Said Soud Said katika Ukumbi wa Sanaa uliopo Rahaleo Zanzibar amesema  hujma hizo zilizoandaliwa na UKAWA  za kufanya maandamano makubwa ya kupinga Serikali iliopo madarakani zilizopangwa nchi nzima zina lengo la kuvuruga amani nchini.
Amesema  Jeshi la Polisi na Wananchi kwa ujumla wametakiwa kuwa macho kutokana na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa siasa za kutaka kuchafua kwa makusudi na kuipeleka nchi katika vurugu jambo ambalo litasababisha kuwepo vitendo vibaya ikiwemo ubakaji na mauaji.

 Aidha amesema Zanzibar haiwezi kuvumilia kuingia katika vurugu hivyo Wananchi wasikubali kushawishiwa na Wanasiasa wasiopenda maendeleo wanaotaka kuvuruga amani iliopo.
“Vijana msikubali kushawishiwa na Wanasiasa wamejitokeza kwa ajili ya biashara hivyo natoa indhari hii kwa kuwatahadharisha wazanzibari wenzangu kuachana na hujuma hiyo inayoandaliwa,”Alisema Said Soud.
Hata hivyo amewaasa Vijana kutokubali kushawishiwa na Wanasiasa kushiriki katika vurugu na badala yake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za kiuchumi na maendeleo kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Akizungumzia suala la amani na utulivu Pemba Mwenyekiti huyo amefahamisha kuwa hali sasa ni yakuridhisha kutokana na kupungua kwa kasi vitendo vya hujumaVisiwani humo na.
“Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Serikali wamesaidia kwa kiasi kikubwa na kuwadhibiti wale wote walioshiriki kufanya vitendo hivyo kwa kuchukuliwa hatua za kisheria,” ameeleza Mwenyekiti huyo .
Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo ameipongeza Serikali iliopo madarakani kwa kuchukuwa hatua nzuri ya kuimarisha Mji wa Zanzibar pamoja na Wafanya Biashara wa Darajani kwa kuitikia agizo lililotolewa na Serikali  la kuhama katika maeneo yao ya kufanyia biashara  na kuwataka kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki ujenzi.

No comments: