Mahakama yatupilia mbali mapingamizi manne yaliyowekwa na Mawakili wa shirika la nyumba la taifa(NHC) Katika kesi ya*
*MBOWE Hotels Ltd t/a BILLICANAS*
Mahakama kuu kitengo cha ardhi imetupilia mbali mapingamizi manne ya kisheria yaliyowekwa na mawakili wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) likiongozwa na wakili sekule.
Mahakama imeshawishika na hoja zilizojibiwa na jopo la mawakili likiongozwa na *Peter Kibatala* Kuwa hoja hizo hazina mashiko kisheria.
Judge wa Mahakama Kuu ameshawishika na kesi mbalimbali ambazo zimetumiwa kushawishi mahakama isizitilie maanani MAPINGAMIZI Hayo.
Imesema vifungu ni sahihi na njia iliyotumiwa na mawakili wakiongozwa na *PETER KIBATALA* ni sahihi
Pia Kuhusu Mkataba imesema hilo suala linabishaniwa na linahitaji ushahidi na Mahakama haiwezi kulichukulia juu kama NHC wanavyotaka
TENA Kuhusu madai ya NHC kuwa Mkataba wa umiliki wa pamoja(JOINT VENTURE) wa Jengo kati yake na Mbowe kumalizika 2015; mahakama imesema hilo suala linabishaniwa na linahitaji ushahidi na Mahakama haiwezi kulichukulia juu kama NHC wanavyotaka
Judge amesema ameshindwa kushawishika na hoja na hata sheria ambazo mawakili wa shirika la nyumba wamezitumia.
Kesi hiyo itaendele tarehe 27/9/2016 katika mahakama hiyo kwa kusikiliza maombi ambayo Mawakili wanomuwakilisha Mbowe Hotels Ltd
Ambayo mojawapo ni kurudisha vitu ambavyo NHC na Dalali wamevitoa sehemu yenye mgogoro kama ambavyo vilikutwa!.
Reporter.
No comments:
Post a Comment