Monday, October 3, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara katika Hospitali za Wilaya ya Iramba Mkoani Singida

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya pamoja na Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.

Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.

“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato umekuwa rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara,Chumba cha upasuaji (Theatre), Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.

Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10, Dk.Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo.
mwisho

dsc_0565Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisiliza maelekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Iramba, Mkoani Singida wakati alipotembelea chumba cha upasuaji Hospitali hapo.
dsc_0571Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vya Maabara 

dsc_0559Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba namna wanavyokusanya mapato.
dsc_0584
dsc_0580Jengo la Utawala la Hospitali ya wilaya ya Iramba na juu  ni baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo
Picha chini ni Majengo ya Zahanati mpya ya Kisimba iliyopo Wilayani Iramba.
dsc_0602Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni kwenye Zahanati hiyo Kisimba
dsc_0592Jengo la  Zahanati ya Kisimba
dsc_0587dsc_0603Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimia wenyeji (Hawapo pichani) wakati alipotembelea Zahanati hiyo ya Kisimba
dsc_0589Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na watumishi wa Zahanati hiyo ya Kisimba.
dsc_0593dsc_0596Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha dawa kwenye Zahanati hiyo.

No comments: