SERIKALI YAJIPANGA KUPIMA VIWANJA VYOTE NCHINI,PROGRAM IMEANZIA MOROGORO

Kaimu Kamishna wa Ardhi nchini Mary Makondo akiwakabidhi wanawake kadhaa Bendera ya Tanzania wakati wakijiandaa kuelekea mkoani kilimanjaro kuungana na wanawake wengine Afrika nzima wanaokutana katika kongamano la wanawake la ardhi kujadili kwa pamoja changamoto zao katika umiliki wa Rasilimali ardhi na Maswala ya uzalishaji,Hafla ahiyo imefanyika makao makuu ya Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Dar es salaam
 Serikali ya Tanzania ya awamu ya Tano imesema kuwa imeanza Program maalum ya miaka 10 ya kuhakikisha kuwa k asilimia mia ya Viwanja nchini vinapimwa na kumilikishwa kwa watanzania wakiwemo wakulima na wafugaji na  ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Kaimu Kamishna wa Ardhi nchini Mary Makondo akizngumza na wanawake hao waliokutana naye kwa ajili ya kumkabidhi baadhi ya maazimio ya wanawake wakulima na wafugaji wadogo wadogo nchini pamoja na kumuaga kwa niaba ya serikali kwa ajili ya kuelekea Mkoani Kilimanjaro kuungana na wanawake wenzao katika Kongamano la Ardhi la wanawake.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi Akizngumza katika shughuli hiyo leo Jijini Dar es salaam
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna wa Ardhi nchini Mary Makondo wakati akizngumza na wanawake wakulima na wafugaji wadogo wadogo wakati wa kongamano liliwalowakutanisha na kiongozi huyo kumkabid
hi baadhi ya madai ya wanawake hao kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro katika kongamano kubwa la wanawake wa Afrika nzima litakalojadili maswala mbalimbali ikiwemo umiliki wa ardhi kwa wanawake afrika

Kamishna huyo amesema kuwa Program hiyo ya miaka kumi ya upimaji na umilikaji wa ardhi kwa wakulima na wafugaji na watanzania imeanza katika wilaya tatu mkoani morogoro  wilaya za kilombero,malinyi na ulanga ambapo wanataraji kumaliza kwa miaka mitatu katika wilaya hizo na kuhamia katika wilaya nyingine nchini.

Mary amesema kuwa zoezi hilo linafanyika kwa umakini mkubwa likiwa na lengo la kuipa ardhi uthamani wake na kuwanufaisha hasa wakulima ambao sasa wataweza kutumia ardhi hiyo katika maswala mbalimbali kama kukopa vifaa vya kilimo kwa kuwa watakuwa na hati halali za mashamba yao na itakuwa Rahisi kusaidiwa kinyume na sasa ambapo wakulima wengi wanatumia mashamba ambayo hayajapimwa Rasmi.
Wanawake mbalimbali wakiandamana Katika Viwanja vya TGNP wakiwa na mabago mbalimbali yenye jumbe ya changamoto zao wakati wakimkaribisha Mgeni Rasmi leo
Kauli hiyo ya serikali inakuja huku Takwimu mbalimbali zikionyesha kuwa ni asilimia 20 pekee ya ardhi iliyopimwa nchini inamilikiwa na wanawake nchini jambo ambalo limekuwa kikwazo kikubwa sana katika uzalishaji kwa wanawake hao ambapo kamishna huyo amewakikishia wanawake kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika litasaidia katika kuwamilikisha wanawake wengi Zaidi ardhi na kuwasaidia katika uzalishaji wake.
Aidha katika hatua nyingine Kmishna huyo amepokea Tamko na maazimio mbalimbali ya wanawake hao Zaidi ya mia moja nchini waliomkabidhi kwa ajili ya kuikumbusha serikali changamoo mbalimbali walizonazo ikiwemo maswala ya umiliki wa ardhi na sharia kandamizi ambazo zimekuwa zikiwaminya wanawake katika umiliki wa ardhi.
Zawadi kwa Mgeni Rasmi

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.