Wednesday, February 8, 2017

Wanawake wajasiriamali wa Kisiwa cha Zanzibar wapatiwa mafunzo ya ujasiliamali na Benki ya KCB Tanzania.

Ofisa Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania Aziza Mkwizu, (aliyekaa kulia), Ofisa biashara wa benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Lutfy Said (aliyekaa wapili kulia), Ofisa biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB, Rashid Mshana (aliyekaa wapili kushoto) na Ofisa mawasiliano ya Umma wa Benki hiyo Margaret Makere (aliyekaa watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.

Ofisa Biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania, Rashid Mshana akimkabidhi mmoja wa wanawake wajasiriamali Bi. Rayyan Khelef cheti cha kushiriki semina ya mafunzo hayo. 

Meneja wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania Iddy Mwacha, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hiyo Kisiwani Zanzibar.

Mwalimu wa ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Seif Abdullah akizungumza na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.

Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Daniel Mghwira akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali Kisiwani Zanzibar.


Benki ya KCB Tanzania inaendelea na programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika changamoto zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.
Benki ya KCB imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar  ambapo matawi ya benki hiyo yapo.
Mafunzo haya ni bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi ya mafunzo hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”


No comments: