Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi
hiyo, Jumamosi Aprili 8, mwaka huu Mbeya City itashindana na Ndanda ya Mtwara
kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Majimaji ya Songea itaialika
African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani
Ruvuma.
Mechi nyingine kwa siku ya
Jumamosi Aprili 8, mwaka huu itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera wakati wakati siku ya Jumapili Aprili 09, mwaka
huu Stand United itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa
Kambarage mkoani Shinyanga.
Ligi inatarajiwa kuendelea
Jumatatu Aprili 10, mwaka huu kwa michezo miwili ambako Simba itakuwa mgeni wa
Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilihali Mtibwa Sugar itaialika
Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment