![](https://3.bp.blogspot.com/-pWXo2tyn5E8/WBDm-yGIguI/AAAAAAAA_Ns/IKom1Szew8cFmhEtXQaf9R9j6DoWN6WnACLcB/s640/1.jpg)
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Louis Hakizimana
ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Theogene Ndagijimana akiwa mshika
kibendera wa mstari wa kulia na Jean Bosco Niyitegeka ambaye atakuwa mshika
kibendera mstari wa kushoto.
Mwamuzi wa akiba ambaye pia
atakuwa anatokea Rwanda ni Ruzindana Nsoro wakati Kamishna wa mchezo atakuwa
Ata Elmanan Hassan Osama kutoka Sudan. Waamuzi hao pamoja na Kamishna wa mchezo
wamefikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko Mtaa wa Jamhuri, katikati ya jiji la Dar
es Salaam, Tanzania.
Wapinzani wa Young Africans
ambao ni Alger waliingia ujana usiku saa 3.30 kutoka Algeria kwa ndege maalumu
ya kukodi na kufikia Hoteli ya Holiday Inn. Kwa mujibu wa kanuni, leo Ijumaa
Aprili 7, mwaka huu saa 10.00 jioni watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Mchezo huo muhimu kwa Young
Africans kusonga mbele kama ilivyotokea msimu uliopita kwa kuifunga Sagrada
Esperanca ya Angola na kutinga hatua ya makundi, viingilio vimepangwa kuwa Sh
30,000 kwa VIP ‘A’; Sh 20,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ wakati mzungunguko itakuwa ni
Sh 3,000.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha
msaidizi wa Young Africans, Juma Mwambusi alisema: “Wachezaji wa Yanga wako na
morali wa hali juu na kikubwa tunawaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi
kuishangilia timu hii kwa sababu ni klabu pekee iliyobaki ikiiwakilisha nchi.”
…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment