Sunday, June 25, 2017

ALICHOKISEMA RAYVAN BAADA YA KUPATA TUZO YA BET

Msanii wa bongo flavour toka kundi la WCB wasafi Raymond au maarufu kama Rayvan baada ya usiku wa jana kuweza kuibuka mshindi wa tuzo ya BET Awards na kusababisha furaha kubwa kwa kundi lake akiwemo bosi wake Diamond Platnamz.


Rayvan ambaye aliwekwa kwenye kipengele cha Viewers Choice Best New International Act aliweza kuibuka mshindi na kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania. pia alipenda kuwapa shukrani zake mashabiki wake wote waliompigia kura wa ndani na nje ya Tanzania. 

Na pia shukrani nyingine kubwa zaidi zimueandee Mungu kwa kuwa yeye ni muweza wa yote na yeye ndiye aliyepanga Rayvani kuchukua tuzo hiyo. "kiukweli ukiangalia ni muda mchache takribani mwaka mmoja nimeingia kwenye muziki na nimeweza kuchukua tuzo kubwa kama BET" alisema Rayvan

No comments: