Wednesday, June 21, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA YAFUTURU NA WATEJA WAKE MWANZA


Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Bi. Christine Manyenye akiwakaribisha wateja na wafanyakazi wa Benki ya KCB kwenye hafla ya futari Mwanza.


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB, Bw. Cosmas Kimario akizungumza na wateja na wafanyakazi wa Benki ya KCB Mwanza kwenye hafla ya futari.




Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB, Bw. Cosmas Kimario (wapili kulia) akipata futari pamoja na wateja wa benki hiyo. Hafla hiyo ya futari iliandaliwa na benki ya KCB kwa ajili ya wateja wake Jijini Mwanza.


Baadhi ya wateja wa Benki ya KCB walio kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Jijini Mwanza wakiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo.


Baadhi ya wateja wa Benki ya KCB walio kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Jijini Mwanza wakiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo.



Mjumbe wa Bodi ya Kiislamu wa Benki ya KCB Sheikh Twaha Bane akizungumza na wateja na wafanyakazi wa Benki ya KCB kwenye hafla ya futari Mwanza.



Mkuu wa Huduma za Kiislamu wa Benki ya KCB Bw. Rashid Rashid akizungumza na wateja na wafanyakazi wa Benki ya KCB Mwanza kwenye hafla ya futari.




Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Mwanza Bw, Joseph Njile akiwashukuru wateja na wafanyakazi wa Benki ya KCB kwa kuhudhuria hafla ya futari.


Mwanza, 20th June 2017 – Benki ya KCB Tanzania imefuturisha wateja wake wa Mwanza katika hoteli ya JB Belmont. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Ahmed Msangi, wajumbe wa bodi ya huduma za kiislamu wa benki ya KCB, wafanyakazi na wateja wa benki hiyo.
Akizungumza wakati wa futari hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa futari hiyo ipo ndani ya vipaumbele vya benki kuwekeza katika jamii na kuboresha uhusiano na wateja wake.
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Kimario alisema na kubainisha kwamba tangu ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

“Mwezi huu mtukufu unaamrisha watu kujirudi, kuutambua na kuuheshimu uwepo wa Mungu. Pia unatukumbusha kufanya yale yampendezayo Mungu na ndio maana benki ya KCB tumeona umuhimu wa kukutana hapa jioni hii ili kufuturu pamoja” alisema Kimario.
Bw. Kimario alieleza kuwa, benki ya KCB inakitengo maalumu kwa ajili ya huduma za Kiislamu inayoitwa “Sahl Banking” na huduma hiyo hupatikana katika matawi

yote 14 ya benki hiyo. “Benki ya KCB ndio ya kwanza kuanzisha huduma zinazozingatia shari’ah hapa nchini na inazidi kuimarisha huduma hizo kwa kuzingatia muongozo husika. Huduma hizo bora ni akaunti za biashara kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali, jamii (community account), akiba (savings account), watoto, hijja n.k.
Alimaliza kwa kuwataka wale ambao bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo na kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu.

No comments: