HABARI ZA KIJAMII

Waislamu watakiwa kuwahurumia yatima na kuwapa huduma bora

Waislamu nchini wametakiwa kuwaonea huruma yatima na kuwapa huduma bora za ikiwemo elimu, afya, malazi kama wanavyowahudumia watoto wao bila kufanya ubaguzi wa aina yeyote.
Hayo yamesemwa na jana na Mkufunzi wa Chuo cha Kiislamu cha Hawzat Imam Swadiq Sheikh Ghawth Nyambwa katika futari maalum na mayatima iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sheikh Ghawth ameeleza kuwa katika maamrisho ya dini ya kiislamu kupitia kitabu chake kitakatifu kinasema miongoni mwa nyumba bora ni ile anayoishi yatima na kupewa huduma zinazostahiki, hivyo ni vyema waislamu kutumia fursa hiyo kwa kuwalea mayatima kwani kuna malipo makubwa kwa mwenye kufanya hivyo.
Huku akitolea mfano kuwa mtume wao Muhammad (S.A.W) amebashiri pepo kwa wale watakao watendea wema mayatima kwa kuwalea vizuri.
Sheikh Ghawth amefafanua kuwa endapo mtu atakula mali ya yatima ajue kuna adhabu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yake, hivyo hakuna budi kwa muislamu kulinda mali ya yatima.
  

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.