Friday, June 23, 2017

ITEL YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KITUO CHA CHAKUHAMA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

Kampuni ya simu za mikononi ya Itel Tanzania yatoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha CHAKUWAMA kilichopo sinza moli jijini Dar es salaam ikiwa ni kushirikisha furaha yao katika kuelekea mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Balozi wa Itel Tanzania Irene Uwoya akikabidhi misaada hiyo kwa ajili ya watoto Yatima na ilipokelewa na msimamizi wa kituo hicho Bw.Hassan Hamisi 
Wakiambatana na Balozi wao hapa nchini msanii Irene uwoya,kampuni ya Itel walikabidhi msaada huo mbele ya watoto,viongozi wa kituo na waandishi wa habari  ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kituo hiko kinacholea watoto yatima pamoja na vituo vingine kwa ujumla katika kuhakikisha watoto wanakuwa na furaha pindi wanapopata baadhi ya mahitaji yanayostahili hasa katika maandalizi ya siku kuu ya Eid Al Fitr.

Kampuni iliweza kutoa msaada wa mchele kg 100,mafuta ya kupikia lita 30,sukari kg 25,unga wa sembe kg 50 na chocolate box 1 ikiwa ni sehemu ya vyakula lakini vitu vingine vilikuwa ni Mdaftari 200,kalamu 100,tshirt 50,mikebe ya kuwekea kalamu 50 na vitu vingine vidogo vidogo.


Aidha,mkurugenzi wa itel Tanzania Bw.Saphon Asajile amesema msaada huo unatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya kampuni na wateja wao hivyo kwa yeyote anayetumia simu ya Itel nae amechangia katika kutoa msaada huo.
Baadhi ya watoto Yatima wa kituo cha Chakuhama kilichopo Sinza Moli wakimsikiliza balozi wa Itel Tz Irene Uwoya walipokuwa wakikabidhi msaada kwa kituo hicho mapema leo jijini Dar es salaam


Balozi wa Itel Tanzania Irene Uwoya akikabidhi baadhi ya zawadi kwa watoto Yatima wa kituo cha Chakuwama kilichopo Sinza Moli jijini Dar es salaam
Balozi wa Itel Tanzania Irene Uwoya akiongea na waandishi wa habari pamoja na watoto Yatima wa kituo cha Chakuhama mapema leo jijini Dar es salaam



No comments: