Friday, June 23, 2017

Benki ya I & M yachangia Matenki maalumu kwa Wizara ya afya yenye thamani ya Sh10 milioni.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya I & M, Bw. Baseer Mohammed (wa pili kulia) akizungumza mbele ya Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi wakati akikabidhi msaada wa matanki maalum ya kuoshea mikono (hand washing tanks) pamoja na sabuni zake kwa Wizara ya Afya vyenye thamani ya Sh10 milioni. Wakisikiliza kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja warejareja wa Benki ya I & M, Bi Lilian Mtalina kushoto Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti TPSF.

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi (Wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I & M Bw. Baseer Mohammed wakati benki hiyo ilipokabidhi msaada wa matanki maalum ya kuoshea mikono (Hand-Washing Tanks) pamoja na sabuni, vyenye thamani ya Sh10 milioni kwa ajili ya kusaidia watu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Mkuu wa Idara ya wateja wa rejareja wa benki ya I & M, Lilian Mtali akionyesha mfano wa matumizi ya tanki maalum la kuoshea mikono (hand washing tank) mara baada ya benki hiyo kukabidhi matanki makubwa matano pamoja na sabuni vyenye thamani ya Sh10 milioni kwa Wizara ya Afya katika jitihada za kuendelea kuhamasisha jamii kunawa mikono mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yatokanayo na uchafu wamikono.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abeli Makubi (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya wateja warejareja wa benki ya I & M, Lilian Mtali (watatu kushoto), akifuatiwa, Bi. Anitha Pallangyo, meneja masoko na mawasiliano wa benki ya I & M, mara baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa matenki maalum ya kuoshea mikono kwa wizara ya Afya yatakayotumika kusaidia jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali.

No comments: