Saturday, June 24, 2017

WATANZANIA WAMETAKIWA KUPENDANA NA KUHESHIMIANA BILA KUANGALIA ITIKADI ZA KIDINI AU DHEHEBU KWA MSIMU HUU WA EID - SHEIKH JALALA


Kiongozi Mkuu wa dhehebu la SHIA Ithna Shariya Hemed Jalala, amewasihi watanzania kutobaguana kwa dini,kabila wala dhehebu kwani umoja ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa lolote.
SHIA Ithna Shariya Hemed Jalala akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam
Sheikh Jalala ameyasema hayo leo alipokuwa anawatakia watanzania kusherekea sikukuu ya Eid kwa amani na usalama ambayo inatarajiwa kuwa siku ya Jumapili au Jumatatu kutokana na kuandama kwa mwezi.
Sheikh Jalala amefafanua kuwa lengo la mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kumfanya muumini kuwa mchamungu na kuleta matokeo chanya hata baada ya Ramadhani kwa kuwa na dalili zifuatazo za kupendana, kushikamana, kuvumiliana, kuelewana, na kuwa wamoja bila ubaguzi wa kiitikadi.
Sheikh Jalala ameongeza kuwa ni vyema amanai iliyopo nchini ikaendelea kuenziwa na dini zote zinatakiwa kuhubiri amani na kukemea vitendo vya kigaidi.
"Dini ya kweli huamrisha amani na kukemea mambo mabaya" alieleza Sheikh Jalala.
baadhi ya waandishi walioudhuria mkutano huo uliofanyika kigogo dar es salaam

No comments: