Friday, September 15, 2017

LHRC YAWANOA WANAHABARI KUHUSU APRM INAVYOFANYA KAZI AFRIKA


Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu LHRC Bi Hellen Kijo Bisimba akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari juu ya mchakato wa KujitathminI kiutawala Bora kwa nchi za Afrika APRM mafunzo yaliyofanyika Leo Jijini Dar es salaam.

Katika Mafunzo hayo wanahabari wamepata nafasi ya kujifunza maswala mbalimbali ya namna mchakato huo unavyofanya kazi Afrika na Tanzania kwa ujumla na Namna Taifa linatekeleza Mchakato huo ikiwa ni moja ya Mikataba ya kimataifa.
Mratibu Tathmin wa Utawala Bora Ndugu Severinius Hyera ambaye alikuwa Muwezeshaji wa Mafunzo hayo akitoa mada mbele ya wanahabari leo Jijini Dar es salaam.

Muwezashaji katika mafunzo hayo ni Katibu Mtendaji wa APRM ambayo ni kifupi cha African Peer Review Mechanism,Bi Rehema Twalib (Pichani)  akitoa mafunzo hayo kwa wanahabari leo ambayo yamefanyika Makao makuu ya LHRC na kudhuriwa na wanahabari mbalimbali.Wanahabari walipata nafasi ya ya kuhoji na kupata maelezo Jinsi mfumo huo unafanya kazi kwa sasa Tanzania.

Picha ya Pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo (Picha zote na Exaud Mtei)

 ELIMU YA APRM ITAKUJIA HAPA HAPA HABARI24 MEDIA

No comments: