Friday, September 15, 2017

WASIOFAHAMIKA WAMEFANYA TUKIO HILI LA KUTISHA TENA

Dereva wa Mbunge John Heche (CHADEMA) amevamiwa usiku wa kuamkia leo Ijumaa Septemba 15,2017  na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga Mjini Tarime ambapo inaelezwa kuwa hali yake siyo nzuri.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku ambapo dereva huyo anadaiwa kukatwa mapanga kichwani.

Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe alipotafutwa kwa njia ya simu na Mwandishi wetu amesema yupo kwenye kikao na akimaliza atatoa ripoti kamili.

Dereva huyo amelazwa katika hospitali ya Bomani Tarime mkoani Mara.

No comments: