Sunday, November 19, 2017

Mothers Helping Mothers kwa kushirikiana na ASBLA waendesha zoezi la uchangiaji Damu kwa Mafanikio makubwa.Ni kuokoa wamama wajawazito

Shirika la Mothers helping Mothers kwa kushirikiana na ASBLA (Ambassadors for Safe Blood and Life Association )Jana walikuwa na zoez lA kuchangia damu katika ofisi za damu salama Msimbazi center.
Katka zoezi hilo wananchi mbalimbali kutoka ndani ya Dar es salaam na mikoa mbalimbali kama mwanza, Tarime, Tanga na Morogoro walijumuika nao katika uchangiaji.
Akizngumza na Mtandao huu mratibu wa zoezi hilo kutoka Mothers Helping Mothers Haiba Msafiri amesema kuwa zoezi hilo limekwenda kwa mafanikio makubwa yaliyochagizwa na idadi nzuri ya watu iliyojitokeza na kufanya kufikia malengo waliyojiwekea ya kuchangia damu.

Ameongeza kuwa zoezi hilo ni moja ya mazoezi muhimu hasa ukizuingatia wanawake wajawazito wamekuwa wakipiteza damu nyingi wakati wa kujifungua hivyo ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa wanachangia damu kuokoa maisha ya wanawake Tanzania.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza wameelezea zoezi hilo kama moja ya njia ya kuisadia jamii kwani damu ni muhimu sana hasa kwa wanawake wajawazito jambo ambalo limewavutia zaidi kushiriki zoezi hilo.
Mratibu Kutoka Mothers Helping Mothers Haiba Msafiri akizngumza na wanahabari juu ya zoezi hilo










No comments: