Wednesday, November 18, 2015

Benkiya I & M yachangia Matenki maalumu kwa Wizara ya afya yenye thamani ya milioni 10

Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya I&M, Bw. Baseer Mohammed (wa pili kulia) akizungumza mbele ya Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi wa kati akikabidhi msaada wa matanki maalum ya kuoshea mikono (handwashing tanks) pampo jana sabuni zake kwa Wizara ya Afya vyenye thamani ya Sh milioni 10 .Wakisikiliza kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja wa rejareja wa Benki ya I&M, Bi Lilian Mtalinakushoto Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti TPSF.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi (Wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M Bw. Baseer Mohammed wakati benki hiyo ilipokabidhi msaada wa matanki maalum ya kuoshea mikono (Hand-Washing Tanks) pamoja na sabuni, vyenye thamani ya Sh. milioni 10 kwa ajili ya kusaidia watu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Mkuu wa Idara ya wateja wa rejareja wa benki ya I&M, Lilian Mtali akionyesha mfano wa matumizi ya tanki maalum la kuoshea mikono (handwashing tank) mara baada ya benki hiyo kukabidhi matanki makubwa matano pamoja na sabuni vyenye thamani ya Sh. miioni 10 kwa Wizara ya Afya  katika jitihada za kuendelea kuhamasisha jamii kunawa mikono mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yatokanayo na uchafu wa mikono.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abeli Makubi (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya wateja wa rejareja wa benki ya I&M, Lilian Mtali (watatukushoto), akifuatiwa, Bi. Anitha Pallangyo, meneja masoko na mawasiliano wa benki ya I&M, mara baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa matenki maalum ya kuoshea mikono kwa wizara ya Afya yatakayotumika kusaidia jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali




No comments: