Tuesday, January 3, 2017
ZITTO KABWE:UHABA WA CHAKULA NI KIBURI CHA SERIKALI
HOTUBA YA KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT Wazalendo NDG ZITTO KABWE KATIKA KATA YA KIWANJA NDEBELE MANISPAA YA MOROGORO JANUARI 2/2017
Hali ya chakula nchini sio nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za vyakula zinapanda kila siku. bei ya sembe sasa kilo moja imefikia tshs 1600 hapa morogoro. Mchele kilo tshs 1500, maana yake leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.
NDOA ZA UTOTONI BADO ZIPO MKOANI IRINGA
Monday, January 2, 2017
ZAHOR: ASANTE PRESIDENT, ILA….
![]() |
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Mbeya City fc , Zahor Pazzy amemshukuru rais wa shirikisho la kabumbu nchini Jamal Malinzi kwa kufanikisha kupatikana kwa hati yake ya uhamisho (ITC) iliyokuwa imekwama nchini DR Congo kwa miaka miwili.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mara baada ya kumalizika kwa mazoezi asubuhi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, Zahor amesema kuwa anafuraha kubwa kuona amerudi rasmi kwenye ulimwengu wa soka baada ya kukaa nje kwa miaka miwili, licha ya jitihada kubwa alizokuwa akizifanya. |
RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO KAGERA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufuatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
KOCHA SALUM MAYANGA KOCHA MPYA WA MUDA TAIFA STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
..…………….……………………………………………………… …………..............
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Haya ndio mambo makubwa yaliyojiri katika soko la hisa kwa mwaka 2016

Kampuni tano ambazo ziliongoza kwa kupanda kwa bei ya hisa zake katika soko la hisa
ACA
|
9810
|
5830
|
68%
|
KA
|
130
|
100
|
30%
|
NMB
|
2750
|
2500
|
10%
|
TOL
|
800
|
760
|
5%
|
JHL
|
10260
|
9530
|
8%
|
Mwaka 2016 tulipata kampuni tatu ambazo zilihorodhesha hisa zake katika soko la hisa la Dar es salaam
Yetu Microfinance
Mufindi Community Bank -MUCOBA Bank
Dar es Salaam Stock Exchange PLC (DSE)
Na kampuni mbili ambazo zilihorodhesha hati fungani zake katika soko la hisa ambazo ni
EXIM Bank LTD
National Microfinance Bank Plc- NMB Bank
Mnamo mwishoni mwa 2016 makampuni matatu ya simu yaliwasilisha maombi ya kuuza hisa na kuziorodhesha katika soko la hisa ambayo ni
Vodacom Tanzania Ltd
MIC (TIGO) Ltd
Airtel Tanzania Ltd
Makampuni haya yanatarajia kuuza na kuhorodhesha hisa zake mwaka huu 2017
DIWANI KAWE, Hitech WATOA MKOPO WA TREKTA, MASHINE KWA WAJASIRIAMALI
Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Kampuni ya Hitech International kwa kushirikiana Ofisi Diwani wa Kata ya Kawe, Mutta Rwakatare, imetoa mkopo wa trekta wenye masharti nafuu ikiwa ni juhudi za kuwajengea uwezo wananchi kujiajiri na kukuza uchumi.
Hitech na ofisi ya diwani huyo zimeingia mkataba wa kuhamasisha wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kumiliki mashine za kutengeneza bidhaa za aina tofauti ili kujiajiri na kukuza kipato chao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi trekta hilo, Mutta alisema kata yake kwa kushirikiana na sekta binafsi inatekeleza kwa vitendo ya uchumi wa viwanda kwa kuwawezesha wananchi kumiliki mashine zinazoongeza thamani ya bidhaa wanazozalisha.
“Kwa udhamini wa ofisi yangu wananchi wa Kawe wanaweza kumiliki mashine waitakayo baada ya kulipa kati ya asilimia 10 mpaka 30 bila kuhitaji dhamana. Hii inasaidia kuondoa vikwazo vya kukuza mtaji vilivyopo kwenye taasisi za fedha na benki,” alisema Mutta.
Kumiliki mashine kutoka Hitech, wananchi wanatakiwa kuwasiliana na ofisi ya diwani huyo ambayo itajiridhisha na makazi na uhalali wa biashara inayofanywa na mwananchi husika kabla hajatimiziwa haja za moyo wake.
Katala Mganga, mkulima wa mpunga aliyepata mkopo huo alisema anatarajia kwenda kuongeza ukubwa wa mashamba kwani gharama za kulima zitakuwa zimepungua kwa kiasi kikubwa na atapata fursa ya kuwasaidia wakulima wengine.
Kwa miaka minne aliyojikita kwenye kilimo hicho, Mganga alisema alianza na eka 10 ammbazo aliziongeza mpaka eka 60 kabla hajapata trekta hilo ambalo anaamini litasaidia kuongeza ukubwa wa shamba lake.
“Ukiwa na trekta gharama za kulima eka moja ni Sh15,000 ilhali ukikodi utatakiwa kulipa zaidi ya Sh50,000. Naishukuru ofisi ya diwani imenisaidia trekta hili,” alisema.
Mkurugenzi wa kampuni ya Hitech International Tanzania, Paul Mashauri alisema kampuni hiyo ina mpango wa kutengeneza ajira milioni tatu mapaka mwaka 2020 jambo litakalofanikiwa kwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini na kati kujiajiri na kuajiri wengine.
“Endapo kila familia itakuwa inaongeza thamani ya bidhaa moja au mbili ama kutengeneza chochote na kukiuza kwa jamii inayoizunguka hili litawezekana. Tunazo mashine za aina tofauti ambazo zinawafaa watu wenye ndoto ya kumiliki kiwanda,” alisema.
Alisema licha ya Kawe, mikopo ya namna hiyo inatolewa Dodoma, Mbeya na Arusha ambako tayari mafunzo yamefanyika. “Kadri siku zinavyoenda tutawafikia wananchi wengi zaidi,” alisema Mashauri.
Kw amujibu wa Mashauri, trekta hilo limegharimu kiasi cha Dola 29,000 za Marekani (zaidi ya Sh58 milioni).
Sunday, January 1, 2017
HOTUBA YA ZIITO KABWE MTONI KIJICHI UZINDUZI WA KAMPENI
HERI YA MWAKA MPYA 2017
Namwomba Mungu, muweza wa yote atupe baraka tele kwenye mwaka huu mpya na kutupunguzia mitihani ya mwaka uliomalizika jana. Tuendeleze Dua na Maombi nchi yetu iendelee kuwa na amani na ustawi katika mwaka huu unaoanza leo.
NAIBU SPIKA AONGOZA MKESHA MKUBWA WA KITAIFA 2017 KWA NIABA YA RAIS DK.JOHN MAGUFULI UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAM
Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Watoto waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao kwenye mkesha huo.
Waumini wakiwa wameinua mikono kwenye mkesha huo.
Maombi yakiendelea.
Wananchi wakisubiri kuupokea mwaka mpya wa 2017 katika uwanja huo.
Shamrashamra za kuupokea mwaka mpya.
Mwaka mpya wa 2017 ukipokelewa.
Wananchi wakiwa wamelala wakisubiri kuupokea mwaka mpya.
ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
Takataka zikipelekwa eneo maalumu.
Takataka zikipelekwa kutupwa.
Waumini wa kanisa hilo wakipiga picha mbalimbali za tukio hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa (kulia), akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipowaongoza waumini wa kanisa hilo kutoa msaada wa magodoro na vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa kanisa hilo.
Kiongozi wa kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa (kulia), akipanda mti.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu (kulia), akipanda mti.
Ofisa Afya wa Hospitali hiyo, Amina Pole (kushoto),
akipanda mti.
Waumini wa kanisa hilo na viongozi wao wakiwa kwenye
tukio hilo.
Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.
| Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada huo. |
UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA MARUZUKU BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM WATOA SARE ZA SHULE KWA WATOTO 200
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.
Mtoto Issa Athumani akipokea msaada huo. Katikati mama yake Halima Issa.
Mtoto Asnat Mashaka akipokea msaada huo. Nyuma yake ni mama yake, Arat Hamisi
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mnyamani Jafari Mrisho (kushoto), akizungumza kwenye tukio hilo.
Katibu Kata wa Kata ya Mnyamani (CUF), Omari Simba (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.
Wazazi na walezi wakiwa na watoto wao wakisubiri kupokea msaada huo.
Vifaa hivyo vikiandaliwa kabla ya kukabidhiwa watoto.
wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.| Watoto na wazazi wao wakisubiri msaada huo. |
Na Dotto Mwaibale
Subscribe to:
Posts (Atom)





