Saturday, December 24, 2016

MBOWE AVUNJA UKIMYA KUHUSU KUPOTEA KWA BEN SAANANE

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema amekuwa kimya muda mrefu kuhusiana na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, msaidizi wake Ben Saanane kwa kuwa suala hilo lipo kwenye uchunguzi. 

Mbowe alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Rukwa. 

Alisema yeye pia ameathiriwa na tukio hilo kama ilivyo kwa wazazi wake na ndugu wengine kwa kuwa ni mtu muhimu kwake katika kutekeleza majukumu yake. 

“Ndugu zangu Watanzania msione nipo kimya, nimefanya hivi kutokana na kuwa suala hili lipo kwenye uchunguzi kwani tukizidisha kuongea ongea wale ambao wamemteka wanaweza kupoteza uhai wake kisa maneno,” alisema Mbowe. 

Alisema, “Chadema ni taasisi ambayo ina vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea kuchunguza tukio hili la aina yake.” 

KINGUNGE : BILA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA,VYAMA VYA UPINZANI VISAHAU KUSHINDA URAIS

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.


Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Friday, December 23, 2016

CHADEMA WABUNI MBINU MPYA YA KUMSAKA BEN SAANANE

Vijana wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa chama cha CHADEMA wakiwa wamevalia Tishet zenye ujumbe wa kumtaka Ben Saa nane akiwa Hai ambaye amekuwa akisakwa kila kona kwa kuhisiwa kupotea yapata mwezi sana.
Habari mbalimbali mitandaoni zimekuwa zikieleza kuwa Ben alipotea bila kujulikana alipo huku wengine wakihisi kuwa  kuwa ametekwa na baadhi ya wapinzani wake kisiasa 

SHAMTE SAFI,NGASSA BADO, CITY VS TOTO KESHO


dsc_0175MAANDALIZI  kuelekea dakika  90 za    mchezo namba 130 wa ligi kuu ya Vodacom  Tanzania bara  kati ya Mbeya City fc na wageni Toto African ya Mwanza  uliopangwa  kuchezwa kesho kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa  yamekamilika.

Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita meneja wa kikosi  cha City, Godfrey Katepa amesema kuwa hali  za  nyota wa timu yake iko vizuri kabisa tayari kwa mchezo huo wa kesho, jambo linaloashiria kuwa hakuna kitakachoizua City kuibuka na ushindi dhidi ya timu hiyo kutoka Mwanza.
Hali ya kikosi chetu ni zuri kabisa, hakuna mchezaji yoyote aliye majeruhi, Haruna shamte aliyekuwa na maumivu ya kifundo cha mguu amerejea kikosi baada ya matibabu ya siku kadhaa jopo la madaktari wetu wametuthibitishia kuwa yuko sawa tayari wa mchezo wa kesho,ni wazi hakuna kinachotuzuia kushinda  mchezo huo alisema.

HABARI24 MEDIA YAPOKEA SALAMU ZA SIKUKUU KUTOKA LAS CONSULTANCY.ASANTEN WADAU

Inline image 2

Thank you for your continued support and partnership. We look forward to working with you in the years to come.
                   Merry Christmas and Happy New Year.

Kocha Azam FC azungumzia ratiba Kombe la Shirikisho Afrika

BAADA ya kuiona ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani iliyotoka juzi jioni, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameweka wazi kuwa amekipanga kikozi chake kufika mbali zaidi kwenye michuano hiyo.

Kwa mujibu wa droo hiyo, Azam FC kwa mara ya pili mfululizo imepangwa kuanzia raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ambapo itakutana na mshindi wa jumla wa mechi ya raundi ya awali kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Azam FC iliyojiwekea malengo ya kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo, itaanza kucheza ugenini na moja timu hizo kati ya Machi 10 hadi 12 mwakani kabla ya kurejeana nyumbani Azam Complex kati ya Machi 17 na 19.
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii wakifuzu hapo, wataingia raundi ya mwisho ya mtoano (play off), watakayocheza na moja ya timu 16 zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikivuka mtihani itaingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Hernandez, alisema kuwa kutokana na usajili uliofanywa na namna kikosi chake kinavyoimarika anauhakika watafika nafasi ya juu zaidi tofauti na malengo iliyojiwekea timu hiyo.
“Tumefurahi namna ratiba ilivyopangwa, tumeanzia raundi ya kwanza kutokana na ubora wa Azam FC tofauti na timu nyingine zilizoanzia raundi ya awali, kiufupi malengo makubwa tumepanga kufika juu zaidi ya hatua ya makundi, namna gani tutafikia ni kutokana na wachezaji waliosajiliwa hivi sasa kuwa na uzoefu mkubwa na ni wachezaji wazuri na tunaamini wanaweza kutufikisha huko tunapokusudia,” alisema.
Kocha huyo alisema kuwa ili kufikia huko, lazima kazi kubwa ifanyike na kila mtu kuweza kujituma kwenye nafasi yake huku akidai kuwa kwa sasa watajitahidi kujipanga vilivyo kwa ajili ya mechi za michuano hiyo ikiwemo kuwafanyia tathimini wapinzani wao ambao mmojawapo wanatarajia kucheza naye.
“Naamini ya kuwa kwa sasa ni muda mzuri wa kujipanga zaidi, haya ni mashindano mazuri na makubwa kinachotakiwa ni sisi kuingia tukiwa tayari tumeshajipanga vizuri, ili ushiriki wetu uweze kuwa mzuri na hatimaye kufika nafasi za juu zaidi,” alisema.

SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI ABADILISHE FEDHA

 Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Jaffar Sabodo akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani na kumshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Sabodo akisisitiza jambo

MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi, Asha Soud ambaye ni mshindi la shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni msanii Haji Salum 'Mboto' Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi msanii Irene Paul.
 Maelekezo ya upokeaji wa zawadi hizo yakitolewa.
 DC Mjema akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi hizo.
 Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
 Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph (kulia) akimkabidhi zawadi Kelvin Mhenzi
Washindi wakiondoka na zawadi zao.

Thursday, December 22, 2016

Chadema waapa kutoibiwa Tena kura ,Lubuva angoka NEC,Mrithi wake afunguka,Lissu alivyohenyeshwa Polisi Jana,magazeti ya leo Dec 23 ijumaa yapo hapa

POLISI WAMHOJI TUNDU LISSU KUHUSU NENO MTAKATIFU RAIS


TUNDULISU AHOJIWA KUHUSU "MTAKATIFU"...


1. Kwanza amehojiwa kwanini anamwita Mheshimiwa Bwana Mkubwa JPM kuwa ni Mtakatifu. Tundulisu amewashangaa Polisi kuwa kwa nini akiita lile jina linalohusiana na udikteta wanamfungulia kesi, Je na hili la Mtakatifu ni shida? Amehojiwa aeleze maana ya Mtakatifu akaeleza ni "asiye na hatia mbele ya Mungu na wanadamu".  

2. Kwanza amehojiwa kuhusu kikosi kazi kinachotesa watuhumiwa wanaokuwa chini ya polisi lakini huchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso na kurejeshwa alfajiri  Central Police.  Amewaambia Polisi kuwa yeye ameongea na walioteswa na wapo tayari kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa kikosi kazi hicho. RCO wa Ilala amekana tuhuma za watuhumiwa kuteswa. 

3. Pili amehojiwa kuhusu sakata la kupotea Ben Saanane na polisi wanavyoweza kumtafuta amewaambia watafute mawasiliano yake ya mwisho waseme Saanane yuko wapi. 

#Note: Lissu amehojiwa chini ya usimamizi wa Wakili Fred Kiwhelo tangu saa Nne asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni hii. Polisi wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu maelezo hayo na Tundulisu ameachiwa.

Hii ni Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Kutoka Polisi aliposhikiliwa kwa masaa kadhaa kwa mahojiano

SHAMTE ‘HATIHATI’ CITY VS TOTO AFRICANS




20161221_104644
WAKATI ‘raundi ya 17 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  ikitaraji kuendelea  jumamosi hii,kikosi cha Mbeya City fc kieendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho ya mchezo  namba 130 dhidi ya wageni  Toto Africans ya Mwanza uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Kwenye mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi, Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema maandalizi kuelekea  mchezo huo  yanaendelea  vizuri na wachezaji wote wakiwa na ari kubwa  licha ya kuwepo kwa taarifa za  majeraha kwa mlinzi Haruna Shamte aliyeumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Kama unavyofahamu jumamosi iliyopita tulipata suluhu ya 0-0 na Kagera Sugar, mara hii tunafanya maandalizi makubwa kuhakiksha  tunashinda mchezo ujao, pointi tatu ni jambo pekee linalohitajika kwenye duru hii ya pili, tunaifahamu Toto kuwa ni timu nzuri lakini mara kadhaa sisi tumekuwa tunaibuka wababe dhidi yao, alisema
Akiendelea  zaidi Ten aliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo dhidi ya Toto, City inaweza kukosa huduma ya mlinzi wake Haruna Shamte aliyepata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo uliopita  ingawa  jopo la madaktari  wameahidi kutoa taarifa  mpya  juu yake siku ya kesho huku akigusia  pia  suala la ITC ya  kiungo Mrisho Ngassa.

20161221_104634Shamte alipata majeraha kwenye mchezo uliopita, huenda  asiwepo kikosini  jumamosi, ingawa hili litategemea na ripoti ya daktari siku ya kesho, kuhusu Mrisho Ngassa ni kweli ITC yake ilichelewa, hii ni kwa sababu ijumaa na jumamosi  ni siku ya mapumziko huko Oman, tulizungumza nao jana wakaahidi kututumia leo, hivyo tuna uhakika leo wataituma na ni wazi atakuwa sehemu ya kikosi  kwenye mchezo huo,alimaliza.

TUNDU LISSU ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI DAR

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,”alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.

Mwandishi alimtafuta Lissu kutaka kujua baadhi ya mambo, ndipo alipopokea simu na kueleza hivyo. Hakuna taarifa zaidi mpaka sasa.

KILICHOMKUTA MWANDISHI WA ITV ARUSHA


Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV mkoani Arusha, Khalfan Lihundi, anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Polisi Usa River, wilayani Arumeru kwa tuhuma za kuandika habari zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.


Lihundi alikamatwa jana jijini hapa majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.