Thursday, June 11, 2015

YAMETIMIA--- NI LIPUMBA TENA MEZANI KWA UKAWA



Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa siku ya Jumapili ya Tarehe 14 mwezi huu wa sita ndiyo siku rasmi ya  kumkabidhi rasmi form ya kuomba kugombea urais wa jamhuri ya muunganoi wa Tanzania mwenyekiti wa chama hicho Profesa IBRAHIM LIPUMBA baada ya kujitokeza mwenyewe katika chama hicho kuomba nafasi hiyo licha ya chama hicho kutangaza kwa muda mrefu watu kujitokeza kutangaza nia.
Naibu Mkurugenzi Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo akizngumza na wanahabari mbalimbali makao makuu ya chama hicho mapema leo juu ya mchakato mzima wa uchaguzi ndani ya chama hicho.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam mapema leo Naibu Mkurugenzi Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo  amesema kuwa chama hicho kilitoa nafasi ya mwanachama yoyote mwewnye nia ya kuomnba nafasi ya kugombea nafasi ya urais kufanya hivyo kuanzia tarehe kumi ya mwezi wa tano lakini hadi kufikia leo asubuhi hakukua na mwanachama mwingine yoyote aliyetangaza nia au kuonyesha nia zaidi ya Mh LIPUMB jambo ambalo amesema kuwa haina budi kukubaliana na hilo na kumkabidhi form hiyo mwenyewe.
Amesema kuwa chama hicho kulikuwa na utaratibu tofauti ambapo kilipanga kuwa baada ya wanachama wote kuchukua form za urais kingewakutanisha kwa pamoja na kuwakabidhi form katika mkutano mkubwa lakini kwa kuwa mwanachama aliyejitokeza ni mmoja haina budi kufanya mkutano huo ambao utafanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa ubungio plaza na kurushwa na television mbalimbali nchini Tanzania.

Katika hatua nyingine mketo amesema kuwa katika nafasi za ubunge na madiwani hadi kufikia sasa chama hicho kimekamilisha uchaguzi katika majimbo 133 kati ya 189 ambapo amesema kuwa mchakato huo unaendelea kuwapata wagombea ambao watapelekwa katika meza ya ukawa na kupatikana wale watakaogombea kupitia UKAWA.

Kwa maana hiyo profesa IBRAHIMU LIPUMBA ndiye atakeyepambanishwa na wagombea wengine wa vyama vya ukawa kumtafuta mgombea mmoja wa umoja huo katika nafasi ya urais

No comments: