Friday, May 2, 2014
HIVI NDIVYO UKAWA ILIVYOFUNIKA PEMBA LEO
Kiongozi wa UKAWA Freeman Mbowe, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
| Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba. |
Mwenyekiti
wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akihutubia katika mkutano wa hadhara
katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia katika mkutano wa
hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
MALAWI YAWASILI, KIINGILIO 5,000/
Timu
ya Taifa ya Malawi (Flames) imewasili jijini Mbeya tayari kwa mechi ya kirafiki
dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Mei 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine.
Flames
ikiwa na msafara wa watu 31 imewasili jana (Mei 1 mwaka huu) saa 1 jioni kwa
njia ya barabara, na imefikia hoteli ya Manyanya. Nayo Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo jijini Mbeya tangu Aprili 27
mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
Kiingilio
katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo
kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu,
Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.
Magari
yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari la wagonjwa, gari la
zimamoto na gari la waamuzi pekee.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
PICHA-MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAZINDULIWA RASMI HUKO KAGERA,TAZAMA PICHA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKIWASHA MWENGE

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za
Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa
Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuhitimisha mbio zake
Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
HAWA NDIO WALIOJITOKEZA LEO NA KUMTAKA RAIS AFUTE KIKUNDI CHA UAMSHO MARA MOJA
Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania dk JAKAYA MRISHO KIKWETE ametakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya kikundi cha mihadhara ya kiislam Tanzania maarufu kama UAMSHO ikiwa ni pamoja na kikifuta kikundi hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kikundi hatari na hakiitakii mema nchi ya Tanzania
Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam
na bw HAMAD TAO ambaye ni mwenyekiti wa taasisi inayojihusisha na kujenga
undugu kati ya dini ya CHRISTIAN AND MUSLIM BROTHER HOOD SOCIETY ambapo katika mkutano na wanahabari mapema leo
taasisi hiyo imesema kuwa kikundi cha uamsho hawana lengo nzuri na nchi ya Tanzania
kuutokana na matamko yake ambayo imekuwa
ikiyatoa ya vitisho dhidi ya watu mbalimbali pamoja na dini nyingine ambapo
amesema kikundi hicho kinasababiosha uhasama baina ya dini na dini.
HAMAD TAO ambaye ni mwenyekiti wa
taasisi hiyo amesema kuwa kikindi cha uamsho hakina tofauti na vikundi vingine
vya kidaidi duniani huku akienda mbali na na kukifananisha na vikundi kama
ALCAIDA,BOCO HARAM NA ALSHABABU.
“sisi tumekuja hapa kwa upendo na
kuipenda nchi yetu tunaiomba serikali ya Tanzania isiwafungie macho hawa watu
wanaounda kikundi hiki kwani ni hatari kwa amani tuliyonayo”alisema TAO
Aidha taasisi hiyo imesema kuwa
tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho matukio ya kigaidi Zanzibar kama kumwagiana
tindikali,makanisa kuchomwa moto na ugaidi mwingine umekuwa ukiongezeka kwa
kasi huku wakikwepa kuwahusisha uamsho moja kwa moja kuhusika na uhalifu huo,
MIGOGORO NDANI YA WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII MCHUNGAJI MSIGWA AIBUKA,SOMA ALICHOZUNGUMZA NA MTANDAO HUU
SIKU moja kupita Baada ya Ikulu ya
Rais Jakaya Kikwete kupuuza maoni ya Kamati ya bunge ya Ardhi,Maliasili na
mazingira ,kwa kitendo chake cha kumrudisha ofisini, Mkurugenzi wa Wanyama
Pori,Profesa Alexander Songorwa,
Ambaye, aliyetimuliwa kazi na Waziri
wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu miezi miwili iliyopita,kwa madai ya
kushindwa kutekeleza Majukumu yake ipasavyo,
EXCLUSIVE INTERVIEW------TANESCO NA SONGAS SASA HAKUELEWEKI,SONGAS WATISHIA KUZIMA MITAMBO YAKE,TANESCO WAIBUKA WAJIBU-SOMA KISA KIZIMA
SIKU chache Kupita Baada,Kampuni ya
kufua umeme kwa njia ya Gesi,Songas limited kutishia kuzima mitambo
yake,kutokana na ilichokiita.shirika la umeme Nchini(TANESCO) kushindwa kulipa
deni linaofikia Dola za Kimarekani 72.8 milioni(karibu sh 116.4 bilioni za
kitanzania).
Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la
Umeme Nchini(TANESCO) Eng Felchesmi J Mramba,ameibuka na kusema Songas
wamevunja makubaliano kwa kitendo chake ,cha kutumia vyombo vya Habari kudai
deni hilo.
Thursday, May 1, 2014
HUZUNIIIII.....MEI MOSI YAINGIA DOSARI, MFANYAKAZI WA IKULU AFIA UWANJANI JIONEE HAPA
Baadhi ya jamaa aliyoambatana nao wakimwangalia mara baada ya kufikishwa chumba cha huduma ya kwanza.
TAARIFA MUHIMU KWA MASHABIKI WOTE WA YANGA
Uongozi
wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi
wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake
Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC
zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani
walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga
kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba
ramba.
SHEREHE ZA MEI MOSI MWANZA ZAFANA
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist
Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa
Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Wafanyakazi wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiingia uwanjani CCM Kirumba Mwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza .
Wafanyakazi wa Idara ya Maliasili wakiingia uwanjani CCM Kirumba katika kuhitimisha siku ya wafanyakazi..
Mahakama ya Tanzania wakiingia uwanja wa CCM Kirumba huku wakitanguliza ujumbe mzito.
Kibanda
cha Veta kilikuwa moja ya vibanda vilivyovutia kwenye maonyesho ya Siku
ya Wafanyakazi zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani
Mwanza.
Wafanyakazi
wa Hospitali ya Bugando wakielekea kuingia kwenye matembezi ya
mshikamano katika kusheherekea siku ya Wafanyakazi kwenye Viwanja vya
CCM Kirumba.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.EvaristWelle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein kushoto anaepunga mkono akiyapokea
maandamano ya Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku
ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini
Zanzibar.
Mashirika
mbalimbali yakipita mbele ya Mgeni Rasmi hayupo pichani katika
Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli
ya Bwawani Mjini Zanzibar.

Mashirika
mbalimbali yakipita mbele ya Mgeni Rasmi hayupo pichani katika
Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli
ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Subscribe to:
Posts (Atom)



















