Friday, June 26, 2015

VIJANA WA MKWASA WAANZA KAMBI RASMI


STARS YAANZA MAZOEZI

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.

Stars inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded Morocco, itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.
Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na leo wamefanya mazoezi asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa na Mudathir Yahya (Azam FC).

CHADEMA NA ACT WAMLILIA MWANDISHI NGULI EDSON KAMUKARA


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAAM ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA EDSON KAMUKARA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa kifo cha aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari mahiri na mhariri wa gazeti la mtandaoni, Mwanahalisi Online, Edson Kamukara, kilichotokea ghafla jana jioni katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ajali ya moto.

Kumwelezea Edson Kamukara ambaye kabla ya kuhamia Mwanahalisi Online linalomilikiwa na Hali Halisi Publishers, alikuwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima, akiwa ametokea Gazeti la Jambo Leo ambalo alijiunga nalo akitokea Gazeti la Majira, katika nafasi hii ya salaam za pole yenye ukurasa mmoja, linaweza kuwa jambo gumu sana.

NAPE AMALIZA MGOGORO WA WAFANYAKAZI WA UHURU PUBLICATIONS LTD - TUMIA HII

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akifurahia jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto), akigana na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kuapata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.

KWA PICHA HIZI ZA LOWASA HUKO MANYARA YANAWEZA KUTIMIA

Msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ukipokelewa kwa shangwe na wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara, wakati alipowasili kwenye mji huo kusaka wadhamini  watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Sehemu ya Wakazi wa Mji wa Babati wakimshangilia Mh. Lowassa pale walipomuona.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na baadhi la viongozi wa CCM Mkoa wa Manyara wakati alipowasili kwenye Ofisi Kuu za Chama hicho, Mjini Babati leo Juni 25, 2015.

ZITTO AKAGUA SOKO KUU WILAYANI MASASI LILOTEKETEA KWA MOTO

1
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akimsikiliza Mwenyekiti wa Soko Kuu wilayani Masasi Mkoani Mtwara, Abdallah Mandoma, lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana, mjini humo ambapo  chanzo cha moto huo kimeelezwa ni hitilafu ya umeme.
2
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akisaidia kuzima moto ambao uliteketeza Soko Kuu la Masasi Mkoani Mtwara, usiku wa kuamkia jana wafanyabiashara zaidi ya 1000 wamepata hassara.
mail.google.com
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akisalimiana na askari aliposhuka kuwapa pole abiria waliopata ajali eneo la Kata ya Mtua Kijiji cha Kilimahewa A, Mkoani Lindi jana, ambapo watu wawili walipoteza maisha. Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi akijaribu kumkwepa muendesha baskeli. (DK)
45
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akizungumza na wananchi wa eneo ilipotokea ajli hiyo

Thursday, June 25, 2015

INAWEZEKANA HUJUI HILI KUHUSU MKE WA KAFULILA NA UBUNGE MWAKA HUU


Inawezekana ulikuwa hujui hili nalokupa kwa sasa--Mke wa Mbunge wa Kigoma Kusini kwa Tiketi ya Chama cha NCCR MAGEUZI Mh DAVID KAFULILA ambaye walifunga ndoa hivi majuzi JESCA KISHOA ni mwanachama wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA na Tayari ameanza harakati zake za kisiasa za kuhakikisha kuwa na yeye anamfuata mumewe Dodoma Mjengomi.

Katika mkutano wa hadhara wa baraza la wanawake la CHADEMA uliofanyika Jijini Dar es salaam hivi juzi mwanamama huyo alipanda jukwaani na kuwasalimia wanawake wa chama hicho huku akionekana kuwa mtu mwenye matumaini makubwa katika harakati zake hizo.

Baada ya kushukua jukwaani mwandishi wa Mtandao huu alipiga naye story kadhaa lakini miongoni mwa mambo ambayo Alitaka kufahamu ni kuhusu jimbo ambalo atagombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu ambapo majibu yake ambayo hakuwa Tayari kuyatoa moja kwa moja alionyesha nia ya kutaka kumtoa mbunge wa  Iramba Magharibi MWIGUKU MCHEMBA ambaye kwa sasa amejikita katika kutafuta nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania.
Kishoa anasema kuwa ana malengo ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la 
 Iramba Magharib kupitia chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA kwa umoja wa UKAWA.
Nilitaka tu nikushirikishe hilo mdau,unaweza kutoa maoni yako




Microsoft Unveils Three additional Smartphones in Tanzania

Kingori Gitahi, Product Manager, Microsoft East Africa 
 Microsoft has today delivered on the promise of optimized productivity for smartphone users with the introduction ofa new range of Lumia phones comprising Lumia 540, Lumia 640XL and the most affordable Lumia device to date, the Lumia 430 Dual SIM in Uganda.

The Lumia 640XL 3G dual SIM will offer users more personal computing and increased productivity through seamlessly integrated Microsoft Office experiences which comes with one year free subscription, OneDrive storage and will retail at Tshs 520, 000.

Also unveiled today was the Lumia 540 Dual SIM for only Tshs 380, 000- a smart choice for value-conscious smartphone buyers. The quality-crafted Lumia 540 Dual SIM features a crisp, clear, 5-inch HD display; 8-megapixel rear-facing camera with LED flash; and 5-megapixel front-facing camera that’s great for taking wide-angle selfies.

Speaking at the launch, Kingori Gitahi, Product Manager, Microsoft East Africa said, “People are looking for a device which brings them more flexibility to switch easily between work and play, without breaking the bank. The Lumia 430, Lumia 540 and Lumia 640 XL offer exactly this.”


The Lumia 540 Dual SIM is a natural choice for people ready to experience their first serious smartphone providing the essentials you need to achieve more every day. On the other hand, with the Lumia 640XL, you can smoothly and quickly access important documents or run all of your favorite websites, apps and games, thanks to the on-board 1GB of memory and powerful quad core Qualcomm Snapdragon processor.


At the same event, Microsoft also unveiled Lumia 430 Dual SIM which becomes the most affordably priced Lumia and will retail at Tshs 220,000. Built with Windows Phone 8.1 software and with a dual-core CPU running at 1.2GHz, you can now use Microsoft Office and Outlookfor work and personal productivity. You can also access up to 30 GB of free cloud storage on OneDrive for safekeeping important content, experience the fun of video calls with Skype-integrated calling and a front-facing camera bringing essential smartphone experiences to budget-conscious buyers.

Tech specs summary:
Lumia 640 XL Dual SIM

Operating system
Windows Phone 8.1 with Lumia Denim
HERE location services
Free global HERE Maps and HERE Drive+Free HERE Transit available in the Store
Display
5.7” HD (1280x720, 16:9) IPS LCD, 294 PPI, Glance screen Corning Gorilla Glass 3. Sunlight readability enhancements
Battery
3000 mAhbattery, removable
Processor
1.2 GHz dual-core Qualcomm Snapdragon 400 processor
Main camera
13 MP AF, LED Flash, Lumia Camera
Front facing camera
5 MP FF
Memory
8GB + free OneDrive[1], micro SD up to 128GB
Dimensions
157.9 x 81.5 x 9mm - 171g


Lumia 540 Dual SIM

Operating system
Widows Phone 8.1 with Lumia Denim
Display
5-inch HD Laminated (1280 x 720, 16:9), 294 PPI
Battery
2200 mAh replaceable
Processor
1.2 GHz quad-core Qualcomm® Snapdragon™ 200 processor
Main camera
8 MP, auto focus
Front-facing camera
5 MP wide angle
Memory
1GB RAM, 8 GB internal mass memory[2]+up to 128 GB Micro SD. OneDrive built-in +30GB free cloud storage[3]
Dimensions
144 x 73.69 x 9.35 mm - 152g

Lumia 430 Dual SIM

Operating system
Widows Phone 8.1 with Lumia Denim
Display
4-inch WVGA (800 x 480, 15:9), 235 PPI
Battery
1500 mAh replaceable
Processor
1.2 GHz dual-core Qualcomm® Snapdragon™ 200 processor
Main camera
2 MP, Fixed focus
Front-facing camera
VGA 0.3 MP
Memory
8 GB + 30 GB OneDrive***, MicroSD up to 128 GB
Dimensions
120.5 x 63.19 x 10.63 mm
127.9g
Operating system
Widows Phone 8.1 with Lumia Denim

“The Lumia 430 Dual SIM continues our commitment to combining the right hardware, software, services and apps with the right price to give people a smartphone they can afford and be proud to use,” Gitahi said.

Microsoft will continue to enhance productivity through mobile phone technologies and continues to build devices that are aimed at enriching the lives of users, while at the same time enabling them strike work-life balance.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONANA NA BALOZI WA ITALY NCHINI TANZANIA KWA MAZUNGUMZO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Italy Nchini Tanzania, Luigi Scotto, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 25, 2015 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Italy nchini Tanzania, Luigi Scotto,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 25, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Ballozi wa Italy nchini Tanzania, Luigi Scotto (wa pili kushoto), baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 25, 2015. Kushoto ni Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Marekani, Balozi Joseph Sokoine (kulia) ni Msaidizi wa Balozi wa Italy, Michelangela Adamo. Picha na OMR


MKOA WA DAR ES SALAAM WAMDHAMINI BERNARD MEMBE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akionyesha fomu zilizojazwa na wanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Shesha (kulia) katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni Juni 25.2015. Kushoto ni mkewe Mama Dorcas Membe. Picha zote na John Badi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 1,500 walimdhamini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiagana na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM 1,500 walimdhamini.


Wednesday, June 24, 2015

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNE 25,2015 HAYA HAPA

MAKUBWA--VYUO HIVI VIMEFUTWA LEO NA NACTE


Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita. 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf B. Rutayuga alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE.
“Kwa kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. 

HALI BADO NI MBAYA KWA WAFANYAKAZI NCHINI TANZANIA-LHRC WAJA NA TAARIFA YA KUSHTUA,SOMA HII

Mwakilishi wa mgeni rasmi GODLISTERN NYANGE (katikati),mkurugenzi wa uwajibikajin na iuwezeshaji kutoka Kituo cha Sheria na haki za Binadamu EMELDA URIO (kulia) na wakili FLAVIAN CHARLES (Kushoto) kwa Pamoja wakiwa wanaonyesha Report ya Taarifa ya Haki za Binadamu na Biashara mara Baada ya kuizindua leo Jijini Dar es salaam
 Imeelezwa kuwa asilimia 99 ya wafanyakazi nchini Tanzania wanafanya kazi chini ya mikataba ambayo hawana ulewa nayo juu ya mgawanyo wa majukumu na kazi zao wawapo kazini
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa taarifa ya haki za binadamu na biashara ya mwaka 2014 iliyozinduliwa leo na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC report ambayo imeeleza changamoto mbalimbali ambazo zinawakumba wafanyakazi nchini Tanzania.
Moja kati ya mambo ambayo yameanishwa katika report hiyo ambayo ilifanyiwa utafiti katika mikoa takribani  kumi na tano nchini Tanzania ni manyanyaso na changamoto mbalimbali ambazo zinawakuta wafanyakazi katika makampuni na sehemu mbalimbali ambapo zimeonekana kuwa kikwazo kikubwa kwa ustawi wa wafanyakazi na shughuli nzima za ajira nchini Tanzania.
Wadau mbalimbali wakikabidhiwa Nakala ya Taarifa hiyo mara baada ya kuzinduliwa leo
Akifafanua mambo ambayo yamegundukika katika tafiti ya report hiyo mmoja kati ya watafiti kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu FLAVIAN CHARLES amesema kuwa maswala ya mikataba kwa wafanyakazi nchini yameendelea kuwa tatizo kubwa ambapo asilmia 99 ya wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi katika mikataba ambayo haielezi wazi majukumu yao halisi huku asilimia 25 ya wafanyakazi walisaini mikataba bila kuwa na makubaliano maalum na waajiri wao.
Aidha swala lingine ambalo limeonekana kuibuliwa na utafiti huo ni hali ya ubaguzi wa walemavu katika maeneo ya ajira ambapo zaidi ya asilimia 70 ya walemavu wanabaguliwa katika maswala ya ajira jambo ambalo limeelezwa kuwa baya sana ikizingatia kuwa walemavu ni watu wanaohitaji msaada wa karibu ili waweze kusonga mbele.


Katika hatua nyingine Report hiyo imeonyesha taifa kutafunwa na tatizo la ukwepaji wa kodi pamoja na biashara ya magendo ambapo imeeleza kuwa nchini Tanzania asilimia kubwa ya makampuni makubwa na wawekezaji wakubwa wenye uwezo wa kulipa kodi wamekuwa wakipata misamaha wa kodi huku watanzania wa kipato cha chini wakishushiwa mzigo huo kwa kuendelea kulipishwa kodi jambo ambalo limeelezwa kuwa linahitaji marekebisho makubwa ili taifa liweze kunufaika na wewekezaji waliopo nchini.
Picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam
Akizungumza wakati wa kuzindua Report hiyo GODLISTEN NYANGE ambaye ni Mkurugenzi wa Tafiti Tume ya sheria haki za binadamu na utawala bora nchini ambaye alimuwakilisha mwenyekiti wa tume hiyo amesema kuwa Report hiyo ya  haki za binadamu katika bishara imegusa eneo ambalo limesahaulika sana na mashirika mengi huku akisema kuwa itasaidia sana kufichua maswala mbalimbali wanayokutana nayo wafanyakazi katika maeneo kazi zao.

WAZIRI BERNARD MEMBE AKUTANA NA WASANII WA FILAMU MKOA WA MOROGORO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini. Picha zote na John Badi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.