Tuesday, October 27, 2015

Hawa ndio wataalam wa CHADEMA wa IT waliokamatwa na polisi,wafikishwa mahakamani leo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (katikati), akizungumza na mmoja kati ya vijana nane waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo, kwa tuhuma za kusambaza matokeo ya kura za mgombea nafasi ya urais wa chama hicho katika mitandao ya kijamii kinyume na utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Imedaiwa vijana zaidi ya 190 walikamatwa kwa kosa hilo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam leo.
Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.

Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo. 


Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo.


Sentens TATA za wakuu wa UKAWA jioni hii mbele ya wanahabari


Wenyeviti wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo chadema ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Hai pamoja na mwenyekiti wa NCCR mageuzi ambaye poa ni mbunge mteule wa jimbo la vunjo pamoja na makamu mwenyekiti wa cha cha democrasia na maendleo chadema Profesa ABDALA SAFARI jioni ya leo wamezungumza na wanahabari kuhusu maswala mbalimbali aambayo yanajitokeza kipindi hiki cha utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania,Hapa nimejaribu kukunukulia baadhi ya maswala muhimu ambayo wamezunguzia hapo.-------------

Orodha Ya Wabunge Zaidi Ya 30 Kutoka UKAWA Hadi Leo


Jimbo la Mlimba Suzan kiwanga wa Chadema ameshinda kwa kura 40,068

Jimbo la Kilombro ameshinda  Peter Ambros Lijuakali wa Chadema ameshinda kwa kura 52,158

Jimbo la Babati mjini Pauline Gekuli wa Chadema ameshinda kwa kura 21,970

Jimbo la Moshi mjini Jaffari Michael wa Chadema ameshinda kwa kupata kura 51,646

Jimbo la Bukoba mjini Wilfred Lwakatare wa Chadema ameshinda

Tarime vijijini akishinda John Heche 

Jimbo la Hai Freeman Mbowe wa Chadema ameshinda

 Jimbo la Buyuni Kigoma ameshinda Kasuku Bilago wa Chadema

Mkinga ameshinda Dustan Kitandulu wa CUF

Jimbo la Tandahimba ameshinda Ahmad Katani wa CUF 





Jimbo la Moshi Mjini Japhary Michael wa Chadema
Jimbo la Monduli Julius Kalanga (Chadema)
 Jimbo Buyungu Bilago Samson Chadema) 
Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema 
Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema
Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 
 Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, 
KAMANDA - Ester N Matiko - Tarime Vijijini

KAMANDA - Ester Bulaya - Bunda Mjini
KAMANDA - Dk. Godwin Mollel- Siha
KAMANDA- Joshua Nassari- Arumeru Mashariki
KAMANDA - Frank Mwakajoka - Tunduma


Mgombea Ubunge Jimbo la Mikumi (CHADEMA), Joseph Haule (Prof Jay), ameshinda Ubunge kwa jumla ya kura 32259 na kutangazwa rasmi kuwa mshindi wa Jimbo hilo

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chadema, Saed Kubenea ametangazwa rasmi mshindi katika jimbo hilo na kumshinda Dr.Didas Masaburi wa CCM

Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Antiphas Mughwai Lissu ametangazwa rasmi mshindi katika jimbo hilo

TAARIFA TATU KUTOKA TFF LEO


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakoingia kambini Jumapili jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam, na marudiano kufanyika Novemba 17 nchini Algeria.
Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini Omani kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 dhidi ya Algeria.
Katika kikosi hicho, Mkwasa amewaita wachezaji wapya sita wakiwemo Salim Mbonde, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Malimi Busungu, Ramadhani Kessy na Malimi Busungu na kufanya idadi ya wachezaji 28.
Wachezaji aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam), Walinzi wa kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo ni Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa pembeni Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars – Afrika Kusini).
Washambuliaji wa kati ni John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – Congo DR).

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi ya tisa huku kila timu ikisaka ushindi wa pointi tatu muhimu.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha Coastal Union kutoka jijini Tanga, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand United uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Wachimba Almasi wa Mwadui FC watawakaribisha Yanga SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto African watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, huku watoza ushuru wa jiji la Mbeya katika uwanja wa Sokoine Mbeya City watakua wenyeji wa Majimaji kutoka mkoani Ruvuma.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa michezo miwili kuchezwa, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa African Sports katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, JKT Ruvu watakua wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.
Awali Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.

Monday, October 26, 2015

MATOKEO RASMI MAJIMBO 10



Hali ya Zanzibar sio Swari,Tizama picha hizi


Hali  ya  Usalama  Zanzibar  sio  nzuri, Polisi  wameizingira  Ofisi kuu  ya  CUF  baada  ya  mgombea  urais  wa  chama  hicho,Maalim Seif Sharif  Hamad  kujitangaza  mshindi  dhidi  ya  mpinzani  wake  ambaye  Dr All Mohamed  Shein

Hali  sio  nzuri katika mji wa Chake Chake, hii ni baada ya vijana   wa  CUF  kuingilia  barabarani  wakidai  wanashangilia  ushindi wa  mgombea  wao  wa  Urais.

  
FFU  wameingilia  kati, wakatoa  maonyo  wakiwataka  wananchi watawanyike  lakini  wakakaidi, ndipo  nguvu  ya  ziada  ya  mabomu  ya  machozi  ilipotumika

Soma kauli ya LOWASA kwa wanahabari mchana huu


Nimewaita kueleza masikitiko yetu mawili haswa katika upande wa jeshi la Polisi. Tuna vijana wetu wanaofanya kazi za IT kwa kujitolea maeneo ya kinondoni na kijitonyama jumla ya vituo vitatu. Hawa vijana wanafanya uzalendo,kushiriki katika uchaguzi wa nchi yao,na kujenga historia moya ya nchi yao,tendo la kuwakamata si la haki kabisa


Wamewavamia na kuwakamata kwa kosa la human trafficing ambalo ni kosa kubwa na halifanani na kazi wanazofanya. Nimeona taarifa zao za matokeo ya kura wameanza kuonyesha watu taratibu zinazompendelea Magufuli. 


Ningependa kuwashauri tume watoe matokeo yote kwa pamoja, Sio kufanya kama hivi wanavyotoa kidogo kidogo yanayoongelea upande wa pili kushinda,wanafanya maandalizi ya kisaikolojia (psychological preparedness) kudhoofisha morali ya wafuasi wa UKAWA ambayo si haki

Swali;

Give us your view So far on the tallying 
Jibu;

So far so good. Ila napenda kutoa pongezi kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi kupia kura,
Wamekua watulivu na kuheshimu sheria na kanuni.
Swali;

You said the main tallying station has been raided, Do you have an alternative?
Jibu;

We have no alternative, we have been handicapped
They have been so unfair
I wish i could charge them in ICC
Swali;

Chadema ina mpango gani kuwatoa hao waliokamatwa?
Jibu;

Jumla yao walikua 191 wanajumlisha kura, Sisi hatuna hatua stahiki zaidi ya kuongea na nyie waandishi wa habari mpeleke taarifa hizi duniani, kwamba huu ni uonevu mkubwa.

Matokeo ya uchaguzi yaliyoanza kutangazwa leo yako hapa

Sentensi 11 kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi TACCEO mchana huu

Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia changzi nchini Tanzania TACCEO ambao wanaratibiwa na kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini LHRC umeendelea kutoa tathmini ya maswala kadhaa wanayoyaona katika zoezi nzima la kupiga na kuhesabu kura.Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELLEN KIJO BISIMBA mchana huu akizngumza na wanahabari.Hapa nimekuwekea sentensi kadhaa walizotoa leo hii kuhusu zoezi hilo
1-Maeneo kadhaa ya nchi ya Tanzania  hata baada ya zoezi la kupiga  kura waliendelea kupiga kura hata baada ya muda kumalizika lakini wengi walimaliza kwa muda husika

2-Swala la kuhesabu kura—90% kura ziolihesabiwa vituoni lakini asilimia moja hazikuhesabiwa vituoni

3-Swala lingine ambalo limerepotiwa na mawakala wetu walioko nchi nzima ni kuwa 99% ya mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu waliruhusiwa kuwepo kwa mujibu wa sheria wakati wa kuhesabu kura.

4-Pia 99% wa ccm na Chadema walikubaliana na matokeo na kutia saini katika nakala za matokeo.

5-Wakati wa zoezi la uhesabuji kura vijana waliokuwa wanasubiri matokeo katika mitaa mbalimbali ya nchi walikabiliana na polisi na mabomu tukio ambalo pia leo limejitokeza katika maeneo ya Temeke ambapo baada ya wasimamizi kuchelewesha matokeo kubandika wananchi walikusanyika na kutaka kupewa matokeo yao jambo ambali lililazimu polisi kuwatawanya kwa mabomu.

6-Mchana wa leo pia huko Zanzibar mabomu yamepigwa kutokana na sakata ambalo limeibuka leo ambapo mgombea wa chama cha wananchi CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD alitangaza kuwa ameshinda uchaguzi huo kutokana na matokeo ambayo ameletewa na mawakala wa chama chake hivyo watu kulipuka na furaha hali ambayo imezua tafrani huko Zanzibar.

7-Nia rai yetu kuwa zoezi la uhesabuji wa kura likafanyika kwa umakini mkubwa na ili kuepusha fujo na hiyo inasababisha watu kukosa uvumilivu na kujitangazia matokeo wenyewe na kusababisha rapsha mitaani

8-Tunaomba hali ya utulivu na amani lakini tukumbuke kuwa haki ndio tunda la amani na kuelewana.

9-Swala la kujumlisha matokeo sio baya ila kujitangazia matokeo ni mbaya sana kwa sababu wanakuwa wanachochea uvunjifu wa amani.

10-Tuhuma mbalimbali za kukamatwa kwa mabox zinazoenea katika maeneo mbalimbali zinasemwa lakini hakuna ushahidi wa kujitosheleza sana kumtia mtu hatiani kwa sababu tume wamekanusha na kusema kuwa hao watu ni wafanyakazi wa kawaida wa serikali na tume hivyo ni kutokuelewa tu mfano lile tukio la vunjo halijapata udhibitisho.

11-Tatizo ni kwamba wafanyakazi wa tume wanapewa vifaa vya uchaguzi lakini hawapewi usafiri wa kubebea hivyo wanalazimika kubeba na kulala navyo nyumbani hivyo ni hatari sana kwa wafanyakazi hao.

Sunday, October 25, 2015

Matokeo ya Urais kutangazwa ukumbi wa Julius Nyerere International Convention centre kwa awamu tatu leo

 Maandalizi yakiendelea ukumbini hapo
Jinsi screen za TV zitavyokuwa zikitoa matokeo rasmi

Macho na masikio sasa yanaangazia ukumbi wa Julius Nyerere International Convention centre  ambako  kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe. Kailima Ramadhani ndipo  matokeo ya Rais awamu ya kwanza yataanza kutangazwa leo  Jumatatu saa 4 asubuhi, saa 7 mchana na saa 10 jioni.

Tizama LOWASA na Mkewe walivyojipigia kura leo

Mgombea urais wa CHADEMA/ UKAWA Edward Ngoyai Lowassa na Mkewe Regina Lowassa wakipiga kura Monduli Jijini la Arusha leo 

Mtiririko wa matukio ya uchaguzi kutoka waangalizi wa ndani TACCEO,leo siku ya kwanza


Wakati zoezi la upigaji na uesabuji kura nchini Tanzania likifanyika katika maeneo mbalimbali nchi nzima mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini wa TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC wamesema kuwa kwa ujumla zoezi hilo limeenda vizuri pamoja na changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza katika vituo vya upigaji kura.


Katika Report yao ya kwanza iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Bi HELLEN KIJO BISIMBA imeeleza kuwa jumla ya waangalizi 1728 walioko mikoa yote nchini Tanzania wamereport zoezi hilo limekwenda kwa utulivu na amani huku wakisema kuwa zaidi ya asilimia 90%.ya vituo vilifunguliwa kwa wakati nchi nzima.

Waangalizi hao wamesema kuwa moja kati ya matukio ambayo waliyapokea kutoka katika maeneo mbalimbali ni pamoja na maeneo kadhaa zoezi la upigaji kura kuchelewa kuanza hadi saa sita mchana ambapo tukio hilo limetokea huko kimara stop over ambapo watu hadi kufikia saa sita walikuwa hawaajaanza kupiga kura.

Tukio nyingine ambalo limerepotiwa nna waangalizi hao ni sakata la mabox 6 ya kupiga kura yaliyokamatwa yaliyokamatwa yakiwa na baadhi ya vifaa vya kupigia kura katika maeneo ya Kilimanjaro kilema kati na makuyuni jimbo la vunjo.

Matukio yote hayo wamesema tayari wameyareport kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

REPORT YA JIONI HII KUTOKA TACCEO

Bdo zoezi limeendelea vizuri kwa kiasi cheke ila maeneo mengine uchaguzi umeahirishwa kutoka huku kituo cha stop over kimara hadi kufikia saa kumi na nusu jioni vifaa vilikuwa havijafika na tume ilikuwa inaahidi kuwa imeagiza vifaa vipo njiani.

Jimbo la mkwajuni wilaya ya kaskazini A mkoa wa kaskazini unguja uchaguzi wa mgombea uwakilishi umeahirishwa baada ya kutokea mchanganyiko wa karatasi za kupigia kura hivyo wananchi waliendelea kupiga kura kwa nafasi nyingine za udiwani,ubunge,na Urais.

Katika kituo cha kujiandikisha cha SACCOS kata ya machanli wilaya ya chamwino jimbo la chilonwa baadhi ya wananchi wameshindwa kupiga kura kwa sababu majina waliyoandikisha kwenye daftari la kudumu ni tofauti na majina ambayo huwa wanatumia hivyo kuwekewa pingamizi la kupiga kura na mawakala wa vyama

Huko magu mkoani  mwanza karatasi zimechanwa zenye majina ya wapiga hura na watu wameshindwa kuona majina yao na limeleta usumbufu mkubwa.
Hadi sasa kuna vituo ambavyo vimemaliza kupioga kura na wanaendelea na zoezi la uhesabiji wa kura.

Katika kituo cha sasi kata ya Mbagata huko arumeru Magharibi vijana walikataa kuwapisha wazee kupiga kura kwa kisingizio kuwa wazee wataikchaguz chama cha mapinduzi.

Mkoani mbeya jimbo la Songwe Kituo cha shule ya msingi mkwajuni kata ya mwambani karatasi za kupigia kura kwa nafasi ya udiwani ziliisha na wananchi wakaendelea kupiga kura kwa nafasi ya urais na Ubunge hii leo.

ENDELEA KUFWATANA NASI KUPATA REPORT NyINGI ZAIDI ----

KITUO CHA SEGEREA MAGEREZA HALI NI SHWARI WENGI WAJITOKEZA KUPIGA KURA

 Wakazi wa Segerea wakiwa katika foleni kwaajili ya kuendelea na zoezi la kupiga kura katika kituo cha Magereza Segerea muda huu huku hali ya usalama ikiwa shwari kabisa
 Foleni ikiwa bado ndefu huku mwamko ukiwa mkubwa kwa rika zote kuanzia vijana na wakina mama na baba zoezi linaendelea vizuri mpaka sasa
 Blogger Josephat Lukaza akiwa katika  foleni ya kupiga kura katika kituo changu cha Magereza segerea kwaajili ya kupiga kura kumchagua kiongozi atakayenifaa