Mbunge wa Arusha mjini mh godbless lema na mbunge wa ubungo Mnyika inasemekana wiki hii wataelekea mtwara kufanya mikutano kwa siku TANO. Ziara hiyo imekuja baada ya kumalizika kwa retreat ya wabunge wa chadema na kamati kuu na kuazimia kufanya ziara ya kikazi na kichama na kuazimia kwenda kuzungumza na wana mtwara. Mnyika atazungumza na wana mtwara kuhusu sera ya majimbo ya chadema na suluhisho la mgogoro wa suala la gesi ambalo kimsingi ndio limechukua sura kubwa kitaifa hivi sasa.