Showing posts with label UZALENDO. Show all posts
Showing posts with label UZALENDO. Show all posts

Thursday, February 15, 2018

Sunday, February 11, 2018

Meya Mwita aungana na wananchi wa jiji la Dar es Salaam kupima magonjwa ya Kisukari na Presha.

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameungana na wakazi wa jijini hapa katika kongamano la  kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha lililoandaliwa na Lions Clubs International kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha Irania  kilichopo jijini hapa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata kipimo cha Presha kutoka kwa Dokta Mahmod Shahamati ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Iranian kilichopo jijini hapa.

Katika kongamano hilo Meya Mwita amewapongeza waandaaji  na kuwaeleza kuwa wasiishie hapo hivyo wafikishe huduma hiyo kwenye halmashauri nyingine za jiji la Dar es Salaam ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo.

Meya Mwita amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kucheki afya zao hususani inapojitokeza fursa hizo kwa kuwa baada ya kupata majibu ya vipimo hivyo inawapa urahisi katika kupata matibabu.

Amesema Taasisi hizo zimekuwa na mchango mathubuti  kwa wananchi kutokana na uzalendo mkubwa waliokuwa nao na hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akijiandaa  kupima Kisukari leo aliposhiriki kongamano la kupima Magonjwa ya Kisukari na Presha
"Jambo hili ni muhimu sana, ninawapongeza, ombilangu kwenu, angalieni namna ya kuendelea kuwasaidia wananchi wengine katika jiji letu la Dar es Salaam, huduma hii ni ya muhimu sana na kila  mwananchi anahitaji kuipata" amesema Meya Mwita.

Awali akimkaribisha Meya Mwita, Rais wa Lions Clubs Shaheen Alam amempongeza na kumueleza kuwa  wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Afya cha  Iranian kwa lengo la kuwasaidia wananchi kutambua afya zao.

Imetolewa leo Februali 11 na  Christina Mwagala Afisa Habari Ofisi ya Meya wa Jiji. 

Friday, February 9, 2018

BULYANHULU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 75,649,524 KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE

Meneja Mkuu wa Migodi wa  Bulyanhulu Benedict Busunzu akikabidhi hundi ya milioni 75,649,524  kwa Mkuu wa wilaya ya   Nyangh’hwale  Hamim Gweyama  kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya wilaya ya hiyo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2017.


Meneja Mkuu wa Migodi  wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale  ambapo alisema Acacia itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi .

Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Bulyanhulu baada ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale.




Na,Joel Maduka ,Nyang'hwale

Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu Acacia kupitia mgodi  wake  wa Bulyanhulu imekabidhi hundi ya shilingi milioni  75,649,524 kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2017.

Akikabidhi mfano wa hundi hiyo  mbele ya madiwani wa halmashauri hiyo Meneja  wa  Mgodi  huo,  Benedict  Busunzu,  alisema  kawaida  mgodi  huo hutoa  ushuru  kwa  Wilaya  mbili  ya   Msalala  na  Nyangh’hwale  kwa  ajili  ya  miradi  ya  maendeleo.

Aidha  alitaja  moja  ya miradi  mingine  ambayo  mgodi  huo  umesaidia  Wilayani  humo  ni  pamoja  na  mradi  wa  mkubwa  wa  kusambaza   maji kwa  wakazi  150,000 wilayani  humo,   wenye  gharama  ya  Shilingi  Bilioni 4.5  ambao  unatarajiwa  kukamilika  mwishoni  mwa  mwaka  huu.

Aidha kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Geita, Celestine Gesimba amewataka madiwani    na watendaji  wa  halmashauri ya hiyo    kuepuka   kutumia  fedha  zinazotolewa  na wadau  mbali mbali    kwa ajili  ya  miradi ya maendeleo  kwa  kulipana  posho  za  vikao,   badala  yake  zote  zitumike  katika miradi  kwa  manufaa  ya  ustawi  wa wakazi  wa Wilaya  hiyo.

“Ninapenda  kuwaonya  viongozi  na watendaji    ambao mpo hapa Nyangh’wale  kuwa  tusitumie hizi  fedha  kwa  ajili  ya kulipana  posho  za  vikao  badala  yake  zote  zietumike  katika  miradi  ya  maendeleo  kwa  jinsi  mtakavyoainisha,”alisema Gesimba.

  Aidha Mkurugenzi  wa  Wilaya  ya  hiyo,  Carlos  Gwamagobe,  pamoja na kushukuru mgodi  mgodi  huo  kwa kuwapatia  fedha  hizo alisema ushuru wa huduma ambayo walikuwa wakipata hapo awali  umeshuka kwani kwa  kiasi kikubwa kwani walikuwa wakipokea milioni mia nne kwa miezi sita .


“Tuna  imani  kuwa  mgodi  huu ukianza  shughuli  zake  kama  ilivyokuwa  awali   hata  ushuru  wa  huduma  utaongezeka  kwani awali  tulikuwa  tukipatiwa  kiasi  cha  Shilingi  Milioni  225   lakini  tangu  kuibuka  kwa  sakata  la  Makinikia,  ushuru  nao  umepungua  mara  mbili  ya  zile  za  awali,”alisema Gwamagobe.

Wednesday, February 7, 2018

MCHUNGAJI MSIGWA AIBUKA NA HILI KWA WAZIRI KIGWANGALA

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Peter Msigwa amefunguka na kumchana Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na kudai kuwa anafanya kazi kwa mizuka na mihemko na kuisumbua sekta ya Utalii na Maliasili nchini.
Tokeo la picha la MCHUNGAJI MSIGWA
Msigwa amesema hayo wakatii alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, mjini Dodoma na kudai kuwa Mawaziri vijana wamekuwa na mihemko.

"Niwashauri hawa Mawaziri vijana fursa 'opportunity is atrracted by talent, skills, perfomance and abillity. Show your talent and abillity,m people will love you' 

"Hawa Mawaziri wa zamani hawa kwa mfano Lukuvi, Tizeba tunawaona wakijibu hoja wanajibu hoja siyo za kimihemko kiasi kwamba unaridhika hata Waziri akikujibu unapenda lakini Mawaziri vijana wengi mnaonekana mnayofanya katika Serikali hii kiasi kwamba Serikali ijayo muonekane hamna tija" kwa sababu mna mihemko sana"

Mbali na hilo Msigwa alikwenda mbali zaidi na kumnyooshea mkono Waziri wa Maliasili na Utalii na kudai amekuwa na maamuzi ya ajabu jambo ambalo linapelekea kiongozi huyo kuivuruga Wizara hiyo.

"Utalii huu umejengwa kwa muda mrefu sana na akitokea mtu mmoja anaamua kufanya tu kwa kutafuta umaarufu atauvuruga kwa muda mfupi sana

" Utalii kwenye pato la taifa unaingiza asilimia 20 na forex ni kubwa inatokana na utalii kwa hiyo hicho si kitu kimoja mtu anaweza kuamka leo anasema nimeharibu na hii diplomasia ya kiuchumi inategemea sana na kutabirika, wawezekaji huko nje wanataka kuona kunatabirika wao kufanya biashara zao. 

"Haiwezekani huyu Waziri anatoa amri mpaka mapolisi wanamkataa anashindwa hata kuwasiliana na Waziri wake wa Mambo ya Ndani, huyu huyu Waziri anatoa amri anapingana na Waziri wa Ardhi, huyu huyu Waziri mmoja anapingana na Waziri wa Uvuvi hatuwezi kuwa na Mawaziri ambao wanakuwa na mizuka na kufanya kazi kwa mizuka wote kama tunalipenda taifa letu tufanye kazi kwa kupendana" alisisitiza Mchungaji Msigwa

Wednesday, January 31, 2018

NAPE AENDELEA KUICHACHAFYA SERIKALI

Mbunge Nape Nnauye leo Bungeni ameipa changamoto Serikali juu ya gharama za kuunganisha umeme na kuishauri kuendelea kuchaji elfu 27,000 hata baada ya mradi wa REA kupita ambapo wataanza kuchaji 177,000 kuunganisha umeme.
              Tokeo la picha la NAPE NAUYE
Nape Nnauye ametoa ushauri huo alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwenda kwenye Wizara ya Nishati

"Kwanza niipongeze Serikali chini ya Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri wanayofanya ya usambazaji mzuri wa umeme vijijini hasa REA awamu ya 3, kwa kuwa gharama za kuunganisha umeme wakati mradi unaendelea ni elfu 27,000 na mradi ukipita ni 177,000 na kwa kuwa idadi kubwa na nzuri ya watumiaji wa umeme ni biashara nzuri kwa TANESCO kwanini bei hii isiwe moja ya elfu 27" alisema Nape Nnauye

Hata hivyo Nape Nnauye aliendelea kusisitiza kuwa kama jambo hilo halitawezekana basi REA waendelee na uwekaji wa nguzo na miundombinu na TANESCO wafanye kazi moja ya kupeleka umeme na kukusanya kodi baada ya kupeleka umeme.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati alijibu hoja hiyo na kudai kuwa amepokea ushauri huo wa Mbunge wa Mtama na kuwa atapeleka katika ngazi zingine na kuona Serikali nini itafanya

"Wazo alilosema Kaka yangu Nape Nnauye linapokelewa na litafanyiwa kazi kwani ni la msingi kwa sababu Wizara yetu na shirika letu la TANESCO na wadau wengine wa nishati tunauza bidhaa hii hivyo ni vema tunapouza tupate wateja wengi ili tupate mapato na kuendesha shughuli mbalimbali na uwekezaji mpya wa maeneoya nishati"

Sunday, January 28, 2018

DKT. SHENI "SIWEZI KUONGEZA MUDA WA UTAWALA, MUDA WANGU UKIISHA NTAONDOKA MAPEMA TU".

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amesema hayupo tayari kuongeza muda wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya Zanzibar.
Dkt Shein amesisitiza kwamba, aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar hivyo hawezi kubadilisha muda wa uongozi na hakuna mtu atakayemfanya abadilishe au amvutie yeye kuendelea kukaa madarakani.

Rais Dkt Shein ameyasema hayo jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baaada ya kurejea kutoka kwenye ziara ya wiki moja katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) alipokua ameambatana na mke wake, Mama Mwanamwema Shein.

“Mimi naheshimu katiba ya Zanzibar, na nina heshimu sheria za Zanzibar. Muda wangu ukifika nitaondoka haraka sana. Hakuna atakayenilazimisha mimi nikae, au atakayenivutia mimi nikae”alisema Rais Dkt Shein.

Aidha, Dkt Shein amesema kuwa, alisikia wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi wakizungumza hilo, lakini hawazuiwi kujadili kwani wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, lakini yeye hayuko tayari kuongeza muda.

“Hilo walizungumza wawakilishi barazani, wana haki ya kuzungumza, kwa mujibu wa taratibu zao na sheria zao na yeyote mwingine anaweza kuzungumza. Mimi nilisikia wakati wananzungumza, Mwakilishi mmoja akasema kwamba kuna baadhi ya nchi duniani zina miaka mitano nyingine saba, sasa kwanini na sisi tusiwe na miaka saba!”

Rais Dkt Shein amesema kuwa, suala la miaka saba labda linaweza kuwepo baada ya yeye kutoka lakini hadhani kama kuna jambo kama hilo.

“Mie sijalisema, sitolisema, na hakuna atayanilazimisha niliseme”alihitimisha Rais Dkt Shein, huku akitilia mkazo kwamba, muda wake ukiisha atamchukua mkewe na kumwambia waondoke

Friday, January 26, 2018

ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA YA MWAKA 2017

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) akiongea na Waandishi wa habari wa radio Times Fm wakati akitoa taarifa ya Mafanikio ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2017, kabla ya kukabidhiwa Tuzo na Cheti cha heshima kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo, Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko akipokea Tuzo ya heshima toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa kutokana na utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa jamii na Taifa kwa ujumla (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Picha ya Pamoja, Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (wa nne kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kulia kwake) na (kushoto kwake) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Thursday, November 9, 2017

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WATEMBELEA HIFADHI YA SELOUS KATIKA KUUTANGAZA UTALII WA NDANI KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wametembelea katika hifadhi ya ya Taifa ya Selous ili kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA. Akizungumza mwenyekiti wa umoja huo, Dkt. Liggyla Vumilia alisema kuwa wameamua kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - SELOUS-MATAMBWE, MOROGORO.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
 Ilikuwa ni furaha kila kona.
Treni ya TAZARA ikichanja mbuga.
 Mahojiano yakiendelea ndani ya treni.
 Moja ya pango ambao treni inapita.
 Reli ya TAZARA imenyooka.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
 Makaribisho ndani ya hoteli iliyopo nje kidogo ya hifadhi ya Selous eneo la Kisaki.
 Wakipata chakula cha usiku.
 Nami mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna (kulia) niliweza kuwakilisha vyema na wana-CAAT. Pembeni yangu ni Chris na Yusuph.
 Wazee wa kazi Kaijage (mbele) akiwa na Dr. Heri.
 Wana-CAAT wakipata kifungua kinywa.
 Wana-CAAT wakiwa tayari kuingia mbugani kujionea vivutio mbali mbali. Wana-CAAT wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuingia mbugani.
 Moja ya wanyama wanapatikana hifadhi ya Selous.
 Eneo la Matambwe gate.
 Furaha baada ya kufika eneo la geti kuu.
 Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole akitoa maelezo machache juu ya hifadhi ya Selous. PORI la akiba la Selous ni moja kati ya hifadhi zenye utajiri wa vivutio adimu vya utalii na ambavyo vinapaswa kutangazwa zaidi kwa ajili ya watalii wa ndani na wa nje. Selous ni pori la akiba lenye ukubwa wa kilometa za mraba 54,000 likijumuisha maeneo ya ardhi oevu, misitu ya miombo, tambarare, nyasi za kuvutia, maziwa na mito inayotiririka, vyote vikifanya vivutio vya aina yake mbali na wanyama wa aina mbalimbali. Pori hili la akiba la Selous lilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani likiwa ni pori la kwanza kutengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori katika Bara la Afrika na la pili duniani kwa ukubwa baada ya hifadhi ya pori la Marekani ambalo linaitwa Yellowstone. Poro hili limegawanyika katika kanda 8 kiutawala. Umaarufu wa Selous si katika wanyama pekee ambao ndiyo kivutio kikubwa cha utalii wa uwindaji, utafiti umebaini kuwa katika eneo la Selous kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya mimea ambayo ikitambuliwa na kutangazwa inaweza kuwa kivutio adimu na cha kipekee cha kitalii.
 Wakisoma ramani mbali mbali inayoonyesha hifadhi hiyo.
 Moja ya ramani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia akizungumza machache na Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole.
 Moja ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya Selous.