Showing posts with label HABARI24 BLOG. Show all posts
Showing posts with label HABARI24 BLOG. Show all posts

Tuesday, February 13, 2018

BRITISH COUNCIL YATOA MAFUNZO YA UONGOZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JIJINI DAR ES SALAAM.


 Meneja Mradi wa Connecting Classroom kutoka British Council,Ephraim Kapungu,akimkaribisha Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni,Kiduma S.Mageni (kulia) kufungua mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji kwa walimu wa shule za msingi na sekondari yaliyofanyika katika Kituo cha Walimu cha Mzimuni kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Elisa Shunda


Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni,Kiduma S.Mageni (kulia) akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya uwezeshaji kwa walimu wa shule za msingi na sekondari yaliyofanyika katika Kituo cha Walimu cha Mzimuni kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam leo. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Shirika la British Council Tanzania. Wanaomsikiliza Kushoto kwake ni Meneja Mradi wa British Council nchini,Ephraim Kapungu na Mwezeshaji wa taasisi hiyo,Edwin Shunda.

 Meneja Mradi wa British Council nchini,Ephraim Kapungu akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wakati wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo.


Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni,Kiduma S.Mageni akizungumza katika ufunguzi huo.


NA ELISA SHUNDA - DAR ES SALAAM

Shirika la British Council nchini linawapatia mafunzo ya uongozi walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari ya siku tatu yanayofanyika katika Kituo cha walimu Mzimuni ambapo mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha na kuwaongezea  walimu hao uwezo wa kiungozi na kiutendaji pamoja na maarifa ya kiutawala kwa walimu wenzake anaowaongoza,wanafunzi, wazazi pamoja na jamii inayozunguka shule.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Ofisa Elimu wa  Manispaa ya Kinondoni,Kiduma Mageni amelipongeza Shirika la British Council kwa kujitolea kutoa elimu hiyo ambayo walimu wakuu hao wakiizingatia na kuifanyia kazi kwa vitendo itawaletea matokeo chanya katika shule wanazozisimamia na kuwajengea heshima katika utawala wao pamoja na jamii nzima inayoizunguka shule hiyo.

“Kitendo cha British Council kujitolea kutoa mafunzo ya uongozi ya uwezeshaji kwa walimu wakuu wa shule za sekondari na msingi ni jambo zuri la kuwashukuru sana wanaongeza chachu ya kumsapoti Rais Dk.John Pombe Magufuli katika chagizo la kauli yake ya Elimu Bure hivyo basi ninyi walimu tumieni fursa hii mnayoipata kujifunza mengi katika semina hii na kwenda kuifanyia kazi katika shule zenu mnazoziongoza naamini kwa kutumia mafunzo haya mtaenda kubadilisha fikra hasi kuwa chanya katika shule zenu zitakazoleta matokeo mazuri ya nidhamu,morali kwa walimu wa kufundisha na ufaulu wa kiwango cha juu kwa matokeo ya wanafunzi wenu” Alisema Mageni

Aidha Meneja Mradi wa Connecting Classroom Bwana Ephraim Kapungu kutoka British Council ambao ndio wafadhili wa mradi huo amesema, British Council imekuwa ikifanya kazi na wizara ya elimu katika kuwajengea uwezo wa kiuongozi wakuu  wa mashule, mbinu bora za ufundishaji kwa walimu wa darasani, na kuwawezesha viongozi wakuu wa elimu wakiwemo watunga sera kuhudhuria mikutano mbalimbali ya kielimu ya kimataifa ili kujifunza na kubadilishana mawazo na viongozi wa nchi zingine.

“Sisi British Council kupitia mradi wa Connecting Classroom tumekuwa tukishirikiana na wadau wengine wa elimu pamoja na serikali katika kujengea walimu uwezo wa kuboresha na kutatua changamoto za kielimu zinazowakabili  wanafunzi wenye uhitaji maalumu ili kuhakikisha wanapata fursa ya kupata elimu bora inayoendana na uhitaji wao lakini pia kupitia mradi huu tumekuwa tukiwezesha na kufadhili urafiki wa kielimu kati ya shule za Tanzania na shule rafiki kutoka nchini Uingereza” Alisema Kapungu.

Nao wa wawezeshaji wa mradi wa Connecting Classroom Bw. Frank Mhando na Edwin Shunda wamesema kuwa kupitia mafunzo hayo wanawajengea uwezo walimu katika nyanja za uongozi bora wa mashule, mbinu bora za  kufundishia na ushirikiano wa kielimu ili kuwapa maarifa mapya walimu wapate mawazo mapya ya kuweza kuwasaidia katika uongozi na ufundishaji.

Imeandaliwa na mtandao wa www.timetza.com

Sunday, November 26, 2017

HABARI 24 MEDIA INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA BIG BOSS EXAUD MTEI KUHITIMU DEGREE YAKE YA KWANZA

Imetolewa na Utawala Habari 24 Blog.

Ikiwa siku ya jana  ya tarehe 25 ya mwezi Novemba imekuwa ni siku ya kihistoria kwa kuwa na matukio mawili makubwa la kwanza likiwa ni Fiaesta ambayo mpaka Mh. Rais Magufuli aliifagilia na la pili ni maafari ya chuo cha ustawi wa jamii.

Chuo cha ustawi wa jamii siku ya jana kimefanya maafari yake ya 41 toka kuanzishwa kwake, na wameweza kuhitimu wanafunzi zaidi ya 300 kwa siku hiyo na mmoja wapo akiwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Habari 24 Media bw. Exaud Mtei.

Habari 24 inachukua nafasi hii kumpongeza mkurugenzi wake kwani safari aliyokuwa nayo ya miaka mitatu haikuwa raisi na kwa kuwa aliweza kumtanguliza mungu hatimaye amatimiza kile alichokipanga na tunaendelea kumuombea mungu aendelee kumuongoza amalize Masters na hatimaye PHD.
Mkurugenzi Mkuu wa Habari 24 Bw. Exaud Mtei akiwa katika pozi, mapema jana katika maafari yaliyofanyika Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Wahitimu wakisikiliza kwa umakini hotuba mgeni rasmi.
Muhitimu wa Shahada ya Ustawi wa Jamii Bw. Exaud Mtei akisherehekea siku ya maafari pamoja na wadau  kutoka media rafiki na Habari 24, kama East Afrika tv na Full Habari Media.
Mkurugenzi Mkuu wa Habari 24 Media Exaud Mtei akipewa hongera na Mkurugenzi mtendaji wa Full Habari Ndugu. Selemani Magari mapema jana jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Habari 24 Bw. Exaud Mtei akiwa katika picha ya pamoja na familia yake na wa mwisho kulia ni Selemani Magari Mkurugenzi wa Full Habari Media. 

                         
                          

Monday, September 11, 2017

ALICHOKISEMA DCI KUHUSU DEREVA WA LISSU

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Boaz amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kufika polisi kwa ajili ya mahojiano juu ya tukio la kupigwa risasi kwa kiongozi huyo ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA.

 
Mkurugenzi huyo amesema hayo jana wakati akifanya mahojiano na kipindi cha HOTMIX  ambapo amesema "Polisi inaendelea kumtaka dereva huyo kufika kwa ajili ya kuisaidia Polisi katika uchunguzi wa tukio hilo".

Hata hivyo kuhusiana na dereva huyo (Simon Bakari), Mwenyekiti wa (CHADEMA) Freeman Mbowe jana katika taarifa yake alisema kutokana na dereva huyo kushuhudia tukio la kutisha wameamua kumpeleka Nairobi ili kupatiwa huduma za kisaikolojia 

Akizungumzia muitikio wa viongozi na watendaji mbalimbali wanaoendelea kufika katika Jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano baada ya kutajwa katika taarifa mbili za Kamati za Bunge zilizochunguza Sekta ya Madini ya Almasi na Tanzanite, DCI amekiri kuridhishwa.

DCI Boaz amesema viongozi hao wamekuwa wakifika kwenye  kikosi maalum cha upelelezi ambacho kimeundwa na vikosi vyote vya Upelelezi, na kuongeza kuwa wanaendelea kuhojiwa na kwa wale watakaobainika kuhusika watapelekwa Mahakamani.

Amesema viongozi hao pamoja na wengine watakaofika wataendelea kuhojiwa kufuatia amri ya Amiri Jeshi Mkuu na kufuatiwa na wito wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro aliyetaka viongozi hao kufika kwa ajili ya mahojiano baada ya kutajwa kwenye taarifa za kamati hizo mbili.

Thursday, April 13, 2017

PUMZIKA KWA AMANI MWANAHABARI JOSEPHAT ISANGO


MWANAHABARI JOSEPHAT ISANGO AMEFARIKI MKOANI SINGIDA NA KATIKA UHAI WAKE AMEPATA KUFANYIA KATI VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI KAMA GAZETI LA TANZANIA DAIMA NA MWANAHALISI

MUNGU MWEMA AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA 

AMEN