Saturday, March 31, 2018

BAVICHA WAKIFANYA HIKI KWA VIONGOZI WA CHADEMA WALIOPO MAGEREZANI

Viongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) kesho watasherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa kuwatembelea viongozi wa chama hicho waliopo magerezani.
Tokeo la picha la BAVICHA
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi ataongoza msafara wa viongozi wa baraza hilo watakaokwenda Segerea kumtembelea Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na wenzake.

Amesema wamefikia uamuzi huo kwa lengo la kwenda kuwatia moyo na kuwa nao pamoja.

Amesema viongozi wengine watakwenda Mbeya kwa ajili ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

"Tunataka kusherehekea nao Pasaka na kuwafahamisha kuwa chama kinaendelea, hatuwezi kurudishwa nyuma wala kutetereshwa,"amesema.

Ole Sosopi pia amewataka vijana wa baraza hilo kuwa tayari kupambana kwa ajili ya chama.

Amesema; "Kuna mambo mengi yanaendelea na tunafahamu wazi kuna ajenda ya kutaka kukifuta Chadema, sasa nawaambia hakuna namna chama hiki kitafutwa, tupo imara na tunazidi kuimarika,'

“Vijana kazi yetu ni kulinda chama na kazi hiyo tutaifanya kwa nguvu zote bila woga, hatutaogopa kufa," amesema.

KAMPUNI YA IVORI IRINGA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TOSAMAGANGA

Huu ndio msaada ulitolewa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa kwa ajili ya kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kuwapa faraja ya kusherekea sikuku ya pasaka wakiwa na furaha
Watoto wa kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga wakiwafurahia kupewa zawadi ya pipi ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa ambazo zipo kwenye ubora unaotakiwa
Watoto wa kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga wakiwafurahia kupewa zawadi ya pipi ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa ambazo zipo kwenye ubora unaotakiwa
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa wakifurahi kutumia bidhaa bora kabisa kutoka kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa ambazo zipo kwenye ubora unaotakiwa walipokuwa wameenda kuwatembelea watoto wa kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga

KAMISHNA WA OPERESHENI WA ZIMAMOTO AZINDUA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (kushoto), akiwa ameambatana na mwenyeji wake mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes (kulia), baada ya kuwasili ofisi za Yatch Club kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (wa pili kushoto), akiwa na wakufunzi kutoka nchini Ujerumani na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Wakati wa  uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.

Mkufunzi kutoka nchini Ujerumani Bw. Dan Jungingfer (kulia), akitoa maelekezo ya mbinu za uzamiaji majini kwenye kina kirefu kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Gift Longwe na Konstebo Baltazari Swai. Wakati wa  uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

Mafunzo haya yanayoendeshwa hapa nchini na Wakufunzi kutoka Ujerumani yana lengo la kuwaongezea Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji weledi katika kukabiliana na majanga ya mafuriko na kuzama kwa watu majini haswa kwenye kina kirefu.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

TECNO KUJA NA KAMERA YA AINA YAKE

Kufuatia matoleo ya simu mbalimbali yiliyotangulia, TECNO, imekua ikitajwa tajwa huku ikihusishwa na ujio wa toleo jipya ikikisiwa kuwa ni muendelezo wa matoleo ya Camon, ni ukweli usiopingika kuwa matoleo ya TECNO-Camon yamekua na kamera nzuri zaidi kufananishwa na matoleo mengine


Miongoni mwa vivutizi vinavyoipa simu kipaumbele, bila shaka simu inatakiwa iwe na kamera yenye megapixel kubwa, TECNO, wamelizingatia hilo

Baadhi ya kurasa za mitandaoni zimeihusisha kampuni ya TECNO juu ya ujio wa toleo jipya likipewa jina la Camon kufuatia histoia ya kampuni kuzindua Camon CX mwaka jana miezi kama hii, bado hakujawa na uhakika wa taaifa hizi hivyo ni propaganda tu


Simu hiyo inakadiriwa kuwa na megapixel 16 mbele pamoja na flashi maalum kwa picha za ‘’selfie’’, uwezo wa kupiga picha zenye ubora wa HD, kamera yake ya nyuma kuja na megapixel nyingi zaidi ssambamba na flashi maalum zinaakisi mwanga ili kupata kuendana na mazingira. 



Maswali kuhusiana na ujio wa simu hiyo `yamekua mengi sana pasina kupata majibu yenye uhakika, kamera inayoweza kupiga picha nyingi ndani ya mfupi zikiwa na ubora wa HD?, bado inaniacha na maswali yanayoamsha morali ya kutaka kujua zaidi

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti http//www.tecno-mobile.com

Friday, March 30, 2018

MBINU MPYA ZILIZOBUNIWA NA TGNP MTANDAO ZA KUFIKISHA UJUMBE KWA SERIKALI NA WANANCHI WAKE

Wanaharakati kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika makundi kuweza kujadili changamoto mbalimbali zilizopo nchini na namna ya kuzitafutia ufumbuzi kupitia bajeti ya mwaka 2018/19.

Baadhi ya wanaharakati wakiwa katika kundi wakijadili jambo fulani.

Wanaharakati kutoka kata mbalimbali wakijadiliana kuhusu bajeti ya mwaka 2018/2019 itakavyoweza kutatua changamoto zao.

Meza kuu ikipokea maswali kutoka kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo lililofanyika mapema jana Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia (TGNP).

Mwananchi kutoka kata ya mabibo Anna Sangai akiomba ufafanuzi juu ya swala la kukatika kwa umeme pindi mvua zinaponyesha katika kata nyingi za jiji la Dar es salaam.
Mh. Altho Mwangoa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya wananchi waliohuduria semina hiyo mapema jana makao makuu ya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.

Mh. Jackson Malangalila akijibu moja ya swali alililoulizwa na wananchi akiwa kama muwakilishi wa serikali na kutoa ufafanuzi juu ya mambo kadhaa ambayo wananchi wanaona hayapo sawa na kuamua kuwahoji viongozi wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa duku duku lake katika mkutano huo, akiwa ameshiriki kama mwananchi akiiwakilisha kata yake anayotoka.

Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP kufuatia mfurulizo wa semina zake za kila jumaa tano (GDSS) wamebuni mbinu mpya itakayowawezesha kufikisha ujumbe kwa urahisi kwa serikali na wananchi wake.

Mbinu hiyo iliyobuniwa na shirika hilo ni ya kusimamisha baadhi ya wafanyakazi wake kuwa kama viongozi wa serikali huku wakijibu maswali na kutoa ufafanuzi kwa wananchi kuhusiana na changamoto mbalimbali za kimaendeleo zinazoikabili nchi kwa sasa.

Katika semina hiyo iliyofanyika mapema wiki hii siku ya jumaa tano ya tarehe 29/03/2018 iliyoongozwa na mada isemayo mpango wa taifa wa maendeleo ya budget 2018/2019, Tanzania mpya ya ndoto yangu nitatoka?

Miongoni mwa maswali muhimu yaliyoulizwa na wananchi hao ni kuhusu swala la serikali kuongeza zahanati katika kila wilaya ikiwa zilizopo toka zamani zinalalamikiwa kuwa hazitoi huduma nzuri na vifaa tiba hakuna ikiwemo madawa ya kutosha.

lakini pia swala la utalii lilipata nafasi kubwa kwa wananchi kuhoji kuwa kwanini mpaka leo miundo mbinu haiboreshwi ikiwa barabara za kuelekea mbugani na sehemu nyingine zenye vivutio vya utalii.

katika sekta hiyo hiyo ya utalii ililalamikiwa kuwa inashindwa kujitangaza vizuri hii ikiwa ni hata kusababisha kuonekana kuwa mlima Kilimanjaro upo nchini Kenya na kusababisha nchi hiyo kupokea watalii wengi zaidi kuliko Tanzania ambao ndio wenye mlima wao.

Aidha katika maswali hayo swala la umeme liliendelea kuchukua nafasi kubwa kwa kuhoji kuwa kila siku serikali inaongezea nguvu katika swala hilo lakini bado changamoto za kukatika kwa umeme ziko pale pale hasa katika msimu huu wa mvua je tunavyosema uchumi wa viwanda tutaweza kufanikiwa ikiwa umeme wetu bado wa mashaka mashaka?

Na mwisho kabisa lilikuwa ni swala la hedhi salama kwa mtoto wa kike ambaye anakosa masomo kwa siku 4 mpaka 5 kwa kukosa taulo za na vyumba vya kujihifadhia, wananchi walitaka kujua serikali inalitazamaje swala hili.


WADAU WATARAJIA KITU TOFAUTI KUTOKA TECNO


Kufuatia ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, makampuni mbali mbali yamekua yakija na matoleo tofauti ili kufanya vema sokoni,TECNO wakiwa ndo kampuni pendwa zaidi katika kuzalisha kile kinachomstahili mteja

Tayari pameshakua na minong’ono ya hapa na pale baina ya wadau wa simu janja “smart phone” ikiinyooshea vidole kampuni ya TECNO, kwa kuihusisha kampuni hiyo na ujio wa toleo jipya ambayo ni muendelezo wa Camon

Mbali na picha mbalimbali zilizozagaa mtandaoni zikionesha muonekano tofauti wa simu hiyo mpya kuzinduliwa, tayari kurasa za mitandaoni zimezua mijadala inayokosa majibu sahihi kuhusiana na simu hiyo, baadhi wakiifananisha simu hiyo mpya kutoka TECNO na zile za kampuni ya Samsung na Apple.



Wadau wamekua na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani cha tofauti ambacho TECNO wameweza kukiongeza kwenye toleo hilo jipya

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz

Thursday, March 29, 2018

WARAMI - MAASKOFU MSIKUBALI KUTUMIWA NA WANASIASA

Mkurugenzi wa Taasisi ya Watetezi wa Rasirimali Wasio na Mipaka(WARAMI) Bw. Philipo  Mwakibinga akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo jijini Dar es salaam.

Mkutano ukiendelea.
                                    ANGALIA VIDEO HII KUJIONEA MENGI ZAIDI...
                      

MAONYESHO YA YOUNG SCIENTISTS TANZANIA (YST) 2018 KUFANYIKA MWEZI AGOSTI

Mwanzilishi Mwenza wa  Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland. 
Meza Kuu pamoja na wadhamini wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia udhamini wao 
Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) akizungumza kwenye mkutano huo.
Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
Muonekano wa chumba cha mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MAONYESHO ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe moja hadi mbili mwezi huo.

"Wanafunzi wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda YST kabla ya tarehe 21 Aprili 2018" alisema Kamugisha.

Kamugisha alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia na ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na wanafunzi watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa sayansi wa YST kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.

Alisema onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi kuwapatia ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambao ni Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Karimjee Jinanjee Foundation (KJF)

"Tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF wameongeza kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa YST kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha vijana kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kamugusha aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka huu kwa sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja mbalimbali za kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na ekolojia, saynsi ya jamii na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi zimejikita katika sekta ya afya,kilimo na usalama wa chakula, mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslimu, medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama ambavyo wamefanya kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi wenye ugunduzi mzuri zaidi zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu.

WADAU WA BIMA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KUEPUKA USUMBUFU KWA WANANCHI

Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano wa Bima uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Kampuni za bima nchini zimeshauriwa kuwahudua wananchi kwa ukweli na uwazi na kutoa huduma za kiwango cha juu ili kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi. Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba wakati mkutano wa wadau bima ulioandaliwa African Insurance Digital Banking uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa bima imeanzishwa kwa ajili ya kulinda biashara na mali hivyo wananchi wanatakiwa kuhudumiwa katika kulinda biashara na mali zao huku wakitoa elimu kwa uwazi. Aliongeza kuwa mtu mwenye bima katika biashara au mali likitokea janga haiwezi kuwa sifuri kutokana na kukata bima kwa ajili ya biashara na mali hizo. "Kampuni za Bima ili ziweze kufanya kazi ni lazima zisajiliwe katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi," alisema. Alisema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda sekta ya bima zina mchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi. Nae Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi. Mtavangu alisema kuwa lengo lingine kuu la mkutano wa kuwakutanisha ni wadau ni pamoja na kujadili changamoto zinazowazunguka watoa huduma wa bima kuweza kujadili kwa nia ya kuboresha utoaji wa Bima kwa wananchi. Aidha Mwenyekiti huyo alisema mkutano huo wameuandaa katika kipindi mwafaka katika kwenda na dhamira ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda ambapo watoa huduma wa bima ndiyo fursa ya kufanya kazi na viwanda hivyo katika utoaji wa bima. "Tutaendelea kufanya mikutano zaidi ili katika kuwaweka watoa huduma wa bima kuwa karibu na wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa maonesho ambapo wananchi wanaweza kupata huduma za bima," alisema. Mkutano huo wa pili wa masuala ya BIMA, ilisema kuenda pamoja na maoneshi ya Bima kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo. Nchi zipatazo Tano zimewesha kushiriki katika mkutano huo ni Rwanda, Kenya, Afika Kusini, Nigeria na Tanzania ambao ndiyo wenyeji wa mkutano. Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni za Bima nchini, Sam Kamanga aliyaomba makampuni ya bima kuendelea kutoa bima kwa uaminifu na uwazi mkubwa ili kuweza kujijengea heshima katika jamii. "Nawaomba watoa huduma zote muwe wawazi, na huduma zenu ziwe za kiwango cha juu maana tumekuwa tukipata malalamiko mengi toka kwa wananchi juu ya uzembe mchache ambao umekuwa ukifanywa na kampuni ambazo si waaminifu, hivyo lazima tufuate sheria na kanuni tulizojiwekea," alisema. Alisema kuwa uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya Bima hivyo wasipokuwa waaminifu watashindwa kuhudumia viwanda na taifa likatapa matokeo chanya.

TECNO KUZINDUA TOLEO JIPYA?

Paparazi tayari wameshaanzisha uvumi kama ilivyo ada, ambapo safari hii wakiihusisha kampuni kinara katika uzalishaji wa simu za mkononi TECNO,ikitajwa zaidi midomoni mwa watu, tetesi zaidi zinaihusisha kampuni hiyo pendwa na ujio wa toleo jipya ikiwa ni muendelezo wa jamii ya Camon inayosemekana kuzinduliwa nchini Nigeria, siku na saa bado havikuwekwa wazi.
Inasemekana kwamba simu hiyo itaendana na uchumi wa Afrika ikikadiriwa kuwa na bei nafuu, hivyo nadhani wa Afrika wanacho cha kujivunia.

Swali ni kwamba je ni kweli TECNO watakuja na toleo jipya kama inavyosemekana midomoni mwa wadau mbali mbali, bado hakujakuwa na taarifa rasmi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika

Mara nyingi TECNO inapohusishwa kuhusu toleo jipya bhaasi huwa kweli,je awamu hii TECNO wanakipi cha tofauti? Maswali yamekua mengi yakiacha wadau vinywa wazi wakiwa na shauku ya kutaka kuona ni nini TECNO watakachoingiza sokoni ikiwa ni muendelezo wa Camon.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz

Wednesday, March 28, 2018

MBEYA: MAELFU WAMZIKA KIJANA ALIYEDAIWA KUUAWA KWA KIPIGO CHA POLISI


Maelfu ya vijana mbeya wamemsindikiza kwenye makazi ya milele kijana Allen Mapunda (20) aliyekuwa mfanyabiashara wa machungwa mkoani Mbeya anayedaiwa kufariki muda mfupi baada ya kuachiwa na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema Jeshi hilo halihusiki kwa namna yoyote na kifo cha Allen ambaye anadaiwa alitoka rumande Machi 25, saa 4 asubuhi na ilipofika saa 12 alifariki dunia.

Awali, Mkuu wa Mkoa Mbeya, Amos Makala alimuagiza RPC Mohamed Mpinga kuunda kikosi kazi kitakachochunguza tukio zima lilipolekea kifo cha Allen Mapunda. Amesema kikosi hiko kijumuishe wanafamilia na jamii ambayo inamfahamu Allen kisha kumkabidhi ripoti ili hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.

Kijana Allen Mapunda ambaye alikuwa mkazi wa Kata ya Iyela, anadaiwa alifariki Machi 25, 2018 saa chache baada ya kuachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Mbeya alipokuwa amekamatwa na jeshi hilo.

CHANZO - GLOBAL PUBLISHERS

HIZI NDIYO SALAMU ZA SIKU KUU YA PASAKA KUTOKA KWA IGP SIRRO

Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro anawashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini. 

Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.
Picha inayohusiana
Tunapoelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.

Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya  utulivu.

Wazazi wanatakiwa kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu, pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa  kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.

Vilevile Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.

Nawatakia Pasaka njema.

Tuesday, March 27, 2018

SHIKA NDINGA MWAKA 2018 YAENDA SAMBAMBA NA MIAKA MINNE YA EFM RADIO

Kituo cha radio cha Efm chenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam mapema leo kimekutana na waandishi wa habari lengo likiwa ni
kujadili mambo makubwa mawili.
Magari ya washindi wa mwaka jana wa shindano la shika ndinga mwaka 2017.

Akiongea katika mkutano huu Meneja Mkuu wa Efm radio na Tv E Bw. Dennis Busulwa alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kuufahamisha uma kuwa mpaka kufikia tarehe 2 ya mwezi 4 mwaka huu kituo hicho kinatimiza miaka minne tangu kuanzishwa kwake.

Aliongeza kuwa mbali na sherehe hizo za kutimiza miaka minne lakini pia wako katika mpango kabambe wa kulitangaza shindano lao la shika ndinga mwaka 2018 lotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Aidha meneja Busulwa alisema kuwa katika sherehe hizo za miaka minne ya kituo hicho wataweza kuongeza masafa yao katika mikoa mingine minne ambayo ni Dodoma, Morogoro, Tabora na Kigoma.

Meneja huyo wa Efm alisisitiza kuwa mpaka sasa kituo chao cha matangazo kimekuwa cha kwanza kusikilizwa ndani ya mkoa wa Dar es salaam kwa utafiti uliyofanywa na mashirika binafsi na ni cha pili kusikilizwa kwa maeneo ambayo matangazo yao yanafika.

Ikimbukwe kuwa mpaka sasa Efm inasikika katika mikoa sita ambayo ni Dar es salaam, Pwani, Mbeya, Mtwara,Tanga na Mwanza  na mpaka kufikia siku hiyo ikiwashwa na hiyo minne itakuwa inasikika katika mikoa kumi ndani ya Tanzania.

Kwa upande wa shika ndinga 2018 safari hii mikoa itaongezeka siyo kama ilivyozoeleka kuwa washiriki wanatoka Dar es salaam na Pwani peke yake.

“Kwa mwaka huu wa 2018 shika ndinga itafanyika katika mikoa sita ambayo ni Dar es salaam, Mtwara, Mbeya, Tanga, mwanza na Pwani na kila mkoa zitaweza kutolewa pikipiki mbili na washiriki wa mikoani watagharamiwa na nauli kuja kushiriki fainali itakayofanyika jijini Dar es salaam” alisema Meneje Busulwa

”Katika haya mashindano ya mwaka huu yataweza kuwa na ubunifu tutaweza kumpata mshindi mmoja wa kiume na mmoja wa kike ambao watapewa zawadi ya virikuu kila mmoja, lakini pia washindi wa pili watapewa boda boda kila mmoja hii ikiwa ni njia yetu ya kuwawezesha wasikilizaji wetu katika Nyanja ya uchumi” aliongezea Meneja Busulwa

Na wadhamini wakubwa wa shika ndinga mwaka 2018 ni Shirika la simu  la TTCL, Tatu Mzuka na Chotec wasambazaji wa vilainishi vya shell Advance lakini pia watu watakao shiriki pamoja katika kuadhimisha miaka minne ya Efm radio pamoja na TVE.


Meneja Mkuu wa Efm Radio pamoja na Tv E Bw. Dennis Busolwa akitoa maelezo mafupi kuhusu shidano la Shika Ndinga 2018 pamoja na miaka minne ya Efm Radio.
Meneja Uhusiano wa shirika la simu la TTCL Bw. Nicodemus Tom akitoa ufafanuzi kuhusu bidhaa zao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Efm Radio pamoja na Tv E wakifuatilia mkutano 
Mkurugenzi Mtendaji wa Chotec Bw.Choba John Mumba akitoa ufafanuzi juu ya mahusiano yao na kituo cha utangazaji cha Efm radio.
Afisa Mahusiano wa Tatu Mzuka Bi. Patronila Mtatiro akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam.
Mkutano ukiendelea.
Mshindi wa Shindano la Shika Ndinga mwaka 2017 Bw. Michael Peter akitoa ushuhuda kwa namna alivyoweza kushinda shindano hilo.
Mshindi wa kike wa shindano la Shika Ndinga Mwaka 2017 Bi. joyce Daniel akitoa ushuhuda kwa namna alivyoshinda na amepata faida gani toka ashinde shindano hilo.