Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Monday, March 12, 2018

RAIS NKURUNZINZA ATANGAZWA KUWA KIONGOZI WA KUDUMU MAISHA KATIKA CHAMA CHAKE

Picha inayohusianaChama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.

Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taaarifa fupi ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

Lakini pia chama hicho tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

Kwenye hafla na makundi ya utamaduni ya chama tawala, katibu mkuu wa CNDD/FDD Bwana Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati azimio hilo alolitaka kuwa ni muhimu mno katika uhai wa chama tawala.

Tangazo hili la chama tawala CNDD/FDD kumfanya Rais Nkurunzinza kama Kiongozi Mkuu wa Kudumu linajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu Marekebisho ya Katiba baadae mwezi Mei. Kati ya mambo mengi katiba hiyo ikipitishwa itamuwezesha Rais Nkurunzinza kuweza kuwania Urais mpaka mwaka wa 2034.

Wadadisi wengi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Lakini pia uamzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na haswa viongozi wenye nia pengine ya kuwania nafasi hiyo na hivyo kujaribu kukiepusha chama tawala na mpasuko kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunzinza.

Isitoshe kwa Wachanganuzi wa siasa za bado wanaiona hatua hii ya Rais Nkurunziza kutangazwa Kiongozi wa maisha kama dalili tosha ya jinsi kiongozi huyo alivyokidhibiti chama cha CNDD/FDD.

Chanzo: BBC Swahili

Sunday, March 4, 2018

NKURUZINZA AWATUPA JELA WAWILI BAADA YA KUMCHEZEA RAFU KWENYE MACHI YA KIRAFIKI

Maofisa wawili nchini Burundi wamehukumiwa kwenda jela baada ya Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza kuwashutumu ‘kuchezewa vibaya’ wakati wa mechi ya mpira wa miguu waliyoiandaa.
Rais Pierre Nkurunziza ambaye ni 'Mlokole' wa Kanisa la Evangelical Christian amekuwa akitumia muda wake mwingi kusafiri na Timu yake ya Haleluya FC ndani ya Burundi kwa ajili ya kushiriki mechi mbalimbali.

Inadaiwa kuwa Februari 3, Rais huyu na timu yake walicheza na Timu ya mji wa Kaskazini mwa Kiremba.

Kama kawaida, upande wa timu pinzani ulikuwa ukifahamu kuwa unacheza na rais wa nchi na kukubaliana kuwa mchezo utakaochezwa utakuwa mwepesi, na hata kuweza kumruhusu Nkurunziza kufunga goli.

Lakini kutokana na Timu ya Kiremba kuwa na wachezaji wengi ambao ni wakimbizi kutoka Congo ambao hawakujua kama wanacheza na rais wa Burundi, walikuwa “wakimshambulia mara kwa mara anapokuwa na mpira na kumwangusha mara kadhaa", shuhuda aliwaeleza AFP.

Waliohukumiwa kwenda jela, Juzi Alhamisi ni pamoja na Mratibu wa Kiremba Cyriaque Nkezabahizi na msaidizi wake, Michel Mutama, kwa mujibu wa shirika la habari.

Thursday, February 15, 2018

ALICHOKISEMA JACOB ZUMA BAADA YA KUJIUZULU NAFASI YA URAISI WA AFRIKA YA KUSINI

Hatimaye rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amekubali kujiuzulu baada ya shinikizo kutoka kwa viongozi wa chama chake cha ANC.
Tokeo la picha la JACOB ZUMA
Akizungumza na Waandishi was Habari jana Jumatano Februari 14, 2018 alisema kuwa amechukua maamuzi hayo kwa faida ya taifa lakini hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.
“ANC haiwezi kugawanyika kwa sababu yangu. Kwa hivyo nimefikia uamuzi wa kujiuzulu kama rais wa nchi mara moja. Licha ya kutokubaliana na uamuzi wa chama changu, siku zote nimekuwa mwanachama mwenye nidhamu wa ANC. Nitaendelea kuwatumikia watu wa Afrika Kusini na chama ambacho nimekitumikia maisha yangu yote,”amesema Jacob Zuma.
Awali Chama cha ANC kilimtaka Rais Jacob Zuma aachie madaraka ndani ya Massa 48 .

Thursday, February 1, 2018

MAHAKAMA KUU NCHINI KENYA YAINGILIA KATI SAKATA LA ODINGA

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru kuwashwa kwa vituo vya habari vitatu binafsi na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu.
Juzi, Jumanne matangazo ya vituo vya KTN, NTVna Citizen TV yalizimwa ghafla na serikali baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya kuzima mitambo yao kuepusha vituo hivyo kurusha moja kwa moja mkutano wa kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga kama Rais wa watu wa Kenya ambapo bado haijulikani kama serikali wataifuatilia agizo hilo.

Sherehe ya kuapishwa kwa Raila ilichukuliwa na wengi kama mzaha lakini serikali imeshikilia kuwa kitendo hicho kilikuwa kinakiuka sheria za nchi hiyo na kwamba ni kosa la uhaini hivyo ilijaribu kuhakikisha taarifa hiyo haitawafikia Wakenya wengi ambao wangelifuatilia tukio hilo kupitia matangazo ya runinga.

Okiya Omtata, muwasilishaji mashtaka na mwanaharakati amesema anataka agizo la serikali litangazwe kuwa kinyume na katiba na vituo hivyo vifidiwe.
Wakenya wengi wamekosa matangazo ya runinga kwa siku tatu sasa. Vituo hivyo vilivyoathirika vimedai kupata hasara ya mamilioni ya dola za kimarekani.

Vituo hivyo vya binafsi vinategemea fedha za matangazo ya biashara na hawakuweza kupata fedha hizo kwa siku zote walizokuwa wamefungiwa ambapo Omtata ametaka serikali ilipie hasara za Citizen TV, KTN na NTV.
Kuibuka kwa mitandao ya jamii kumeathiri vyanzo vya mapato vya vituo vingi vya habari na kulazimika kuwafuta kazi mamia ya wafanyakazi wao ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Serikali ya Kenya ilitaka vituo hivyo vifungwe hadi polisi wamalize uchunguzi dhidi ya wanasiasa na waandishi walioshiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Bw. Odinga siku ya Jumanne.

Friday, December 22, 2017

WATU BILIONI 7 DUNIANI WAPINGA AZIMIO LA TRUMP SOMA HAPA KUJUA ZAID

Marekani imefeli  kuulazimisha ulimwengu kukubaliana na azimio lake lililokinyume na sheria, wakati mkutano mkuu  wa Umoja wa Mataifa ulipopitisha kwa idadi kubwa ya wanachama wake,kupinga azimio la Trump linaloitambua Jerusalem kama Mji Mkuu wa Israeli.

Pamoja na vitisho vya Marekani kwa nchi za dunia kuwa itainyima misaada ya kifedha, kupitia Mwakilishi wake katika Umoja huo wa Mataifa kwamba “Aidha fedha au kulipitisha azimio”, Marekani na Israeli pamoja na nguvu zao hazikuweza  isipokuwa kuzikinaisha nchi 7 tu, katika kupigia kura ya hapana azimio hilo zikiwemo zenyewe.

Nchi 128 zimelipigia kura ya ndio azimio hilo,ambazo ni sawa na watu bilioni 7 walio ulimwenguni, sawa na asilimia zaidi ya 90% ya wakazi wote, huku azimio hilo likiwa linalazimisha kuwa kwake, kwa kupata zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wakamati kuu ya mkutano mkuu, likiwa na uzito sawa na maazimio ya Baraza la Usalama.

Tanzania vilevile imepigia kura ya ndio azimio hilo ikiwa pamoja na nchi nyingi duniani, zikiwemo China, India, Urusi, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na idadi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya, nchi zote za kiislamu na kiarabu pia nchi nyingi za  Amerika ya Kusini.


Kilichoshangaza zaidi ni kuona dola ya Vatikani imepinga azimio la Trump, dola ambayo yenyewe  inawakilisha ulimwengu wa kikristo, huku yakiwa makubaliano ya kiislamu, kikristo na kibinaadamu yote yanapinga azimio la Trump lisilo la kisheria na si la kiuadilifu, ambalo pia linakwenda kinyume na kanuni na sheria zote za kimataifa.

Tuesday, November 21, 2017

MUGABE AAMUA KUNYANYUA MIKONO JUU BAADA YA KUONA MAJI YAMEMFIKA SHINGONI

SPIKA  wa bunge la Zimbabwe, Jacob Mudenda   jana ametangaza hatua aliyoichukua kiongozi mkuu ambae ni Rais wa zimbabwe Mh.  Robert Mugabe ya kuamua kujiuzulu.
Image result for MUGABE
Spika huyo amesema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo cha habri cha reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng’oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung’atuka mamlakani wiki hii.

Monday, November 20, 2017

EMMERSON AONEKANA MSALITI KWA MUGABE LICHA YA VYEO VYOTE ALIVYOPEWA RAIS HUYO..

Ni siri iliyofichuka nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kwamba Emmerson Mnangagwa alitaka kumrithi Robert Mugabe kama rais.
Tokeo la picha la Emmerson Mnangagwa
Na Bwana Mugabe anaonekana kuwa amekuwa akichezea hisia zake - na amekuwa akimpandisha vyeo katika chama tawala cha Zanu-PF party na hata katika serikali, jambo lililozusha uvumi kwamba Bwana Mnangagwa ''ndie mrithi wake'' lakini baadaye alimshusha cheo huenda baada ya kuonyesha azma yake wazi pengine kupita kiasi.
Lakini baada ya kufutwa kazi, inaonekana kana kwamba subra ya Mnangagwa anayefahamika kwa jina maarufu la "mamba" ilikwisha.
Baada ya kufutwa kazi na Bwana Mugabe kumpuuza na kumshutumu hadharani kwa "usaliti", wafuasi wake katika jeshi waliingilia kati kwa niaba yake.
Lakini yeyote mwenye matumaini kwamba urais wa Mnangagwa utamaliza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe huenda anajitanganya .
Wakosoaji wake wanasema kuwa Kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 71- ana damu mikononi mwake.
uhusiano wake na Kongo
Bwana Mnangagwa alizaliwa katika jimbo la Zvishavane na anatoka katika kabila dogo ambalo ni sehemu ya jamii ya Washona
Watu wa Kabla la Karanga ni kabila kubwa katika jamii ya Washona na baadhi wanahisi ni wakati wao sasa wa kuingia madarakani, kufuatia miaka 37 ya utawala wa raia Mugabe anayetoka katika kabila la Zezuru

KENYYATA APEWA USHINDI NA MAHAKAMA KUU NCHINI KENYA

Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017
Image result for KENYATA
Kesi hiyo ambayo ilikuwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, iliongozwa na majaji 6 akiwemo Jaji Mkuu David Maraga, na kutoa uamuzi kuwa Uhuru Kenyatta ni mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 26.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama ya Juu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo, na kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa muhula wa pili.

Ikumbukwe uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais ya uchaguzi wa kwanza wa Agosti 8, 2017 na kutaka urudiwe mara ya pili.

Wednesday, November 15, 2017

MUGABE AWEKWA KIZUIZINI, RAIS ZUMO WA SOUTH AFRIKA ATHIBITISHA HILO

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewekwa kizuizini na Jeshi la Ulinzi usiku wa kuamkia jana katika mji mkuu wa Harare, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amethibitisha.
Tokeo la picha la MUGABE
Zuma alisema jana kwamba alipigiwa simu na Mugabe mwenyewe. Taarifa kutoka ofisi ya Zuma ilisema: "Rais Zuma alizungumza na Rais Robert Mugabe mapema leo na amedokeza kwamba anazuiliwa nyumbani kwake lakini alisema yuko salama."

Kuanzia Jumanne wanajeshi walionekana wakivinjari na kupiga doria katikati ya Harare, baada ya kuteka kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Zimbabwe (ZBC) kwa kile kilichoelezwa wanawalenga “wahalifu”.

Hatua hiyo ya jeshi inaweza kuwa ni mpango wa kumwondoa Mugabe na kumweka katika nafasi hiyo makamu wake aliyefukuzwa kazi wiki iliyopita Emmerson Mnangagwa, shirika la BBC limeripoti.

Ofisa mmoja wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alionekana kwenye televisheni baada ya kukiteka kituo hicho akisema Mugabe na familia yake wako “salama na afya njema na ulinzi wao ni wa uhakika ".

Meja Jenerali Moyo alisema, “Sisi tunawatafuta wahalifu waliomzunguka yeye (Mugabe) ambao wanafanya uhalifu na kusababisha machungu ya kijamii na kiuchumi nchini.”

"Mara tutakapokuwa tumekamilisha operesheni hii, tunatarajia kwamba hali itarudi kuwa ya kawaida."

Kufukuzwa kazi kwa Mnangagwa wiki iliyopita kutengeneza njia kwa mke wa Rais Mugabe, Grace kuteuliwa katika nafasi hiyo hivyo kuwa na matumaini ya kuteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha mumewe.

Milio mizito ya bunduki ilisikika kaskazini mwa mji wa Harare hadi jana alfajiri.

Wednesday, October 11, 2017

VITA YA TRUMP NA VYOMBO VYA HABARI BADO INAENDELEA

Rais Donald Trump ameendeleza mgogoro wake na vituo vya runinga nchini humo akisema kuwa vimekuwa na upendeleo na kuonya kwamba atafutilia mbali leseni zao.
Image result for trump wa marekani
Alikasirishwa na ripoti ya ktuo cha habari cha NBC iliodai kwamba kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kwamba alitaka kuongezwa kwa kiwango kikubwa silaha za kinyuklia nchini humo.
Rais huyo alisema kuwa habari hiyo ilitungwa.
Waziri wake wa ulinzi Jim Mattis aliitaja taarifa hiyo kama isiokuwa ya ukweli.
Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita bwana Trump 'mtu mjinga' matamshi ambayo Bwana Tillerson hajayapinga lakini ambayo rais Trump ameyataja kuwa habari bandia.
Wanahabari wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufutilia mbali lesen za vyonbo vya habari.
Zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo.
Lakin baadhi ya makundi ya kupigania haki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

Saturday, July 8, 2017

TANZIA - JENERALI MSTAAFU JOSEPH NKAISSERY AMBAE ALIKUWA WAZIRI WA USALAM WA KENYA AMEFARIKI DUNIA


Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery amefariki dunia.

Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
“Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema.
“Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.”
Jenerali Joseph Kasaine ole Nkaissery, 67, amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G. Kariuki aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.

Friday, July 7, 2017

PATA UNDANI WA PROJECT MPYA YA WIZ KID

Wiz Kid ndiye msanii pekee kwa sasa Afrika anayeongoza kushirikishwa na kushiriki katika ngoma kubwa za wasanii na kupelekea kupata tuzo kama BMA(Billboard Music Awards) ambapo alifanikiwa kunyakua tuzo tatu akiwa na rapper Drake.


Msanii huyo kutoka Nigeria anatarajia kuachia project yake mpya mwezi huu ifikapo tarehe 14, project hiyo inayoitwa “Sounds From The Other Side” (SFTOS) itakuwa na ngoma zipatazo kumi na mbili.
Kupitia mtando wa Instagram msanii huyo ameshare cover ya project yake hiyo itakayo kuwa na ngoma kama ‘Dirty Wine, One For Me, Gbese ngoma ambayo amemshirirkisha Trey Songz.

TANZIA - BRADLEY LOWERY MTOTO ALIYEKUWA MAARUFU KWA KUSHABIKIA SUNDERLAND AFARIKI DUNIA LEO


Kama ni shabiki wa soka la England najua jina la Bradley Lowery sio geni katika masikio yako kutokana na umaarufu wa mtoto aliyekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa kupenda sana kuishabikia Sunderland.
Bradley ambaye alikuwa ana mapenzi na Sunderland amefariki leo baada ya kusumbuliwa na kansa kwa muda mrefu, Bradley alikuwa akimpenda sana mshambuliaji wa zamani wa Sunderland ambaye amejiunga na AFC Bournemouth Jermain Defoe.
Shabiki huyo mtoto wa Sunderland aligundulika kuwa ana kansa akiwa na umri wa miezi 18 lakini amefariki leo akiwa na umri wa miaka 6, taarifa za kifo cha Bradley kimetolewa kupitia mitandao ya kijamii na wazazi wake
.

Friday, May 5, 2017

NYANI ALBINO AOKOLEWA AKISHAMBULIWA NA WANAKIJIJI

Nyani mkubwa albino asiye wa kawaida anatunzwa na kundi moja la kuwalinda wanyama nchini Indonesia baada ya kuokolewa akishambuliwa na wanakijiji.

Nyani mkubwa albino asiye wa kawaida anatunzwa na kundi moja la kuwalinda wanyama nchini Indonesia baada ya kuokolewa.

Nyani huyo wa kike mwenye nywele nyeupe na macho ya buluu alikuwa anazuiliwa katika eneo moja la mashambani nchini Indonesia katika eneo la kisiwa cha Borneo.

Alikuwa amezuiliwa katika kizimba kidogo kwa siku mbili na bado alikuwa akionesha tabia za msituni kulingana na kundi hilo la kuwalinda tumbili la Borneo Orangutan Survival Foundation.

Mnyama huyo huenda akawachiliwa na kwenda msituni ,limesema kundi hilo.

Nyani Albino ni wachache na huyu ni wa kwanza kuchukuliwa na kundi hindi hilo katika historia yake ya miaka 25.Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua yake ishara kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na wanakijiji waliomkamata

Kundi hilo limesema kuwa limebaini kwamba mnyama huyo alikuwa na tatizo la albino baada ya kumfanyia ukaguzi likisema kuwa macho yake yalikuwa hayapendi mwanga mwingi.

Mnyama huyo anayeaminika kuwa na umri wa miaka 5 anachunguzwa katika kituo cha kubadili tabia cha shirika hilo, ambacho kinawahifadhi zaidi ya tumbili 500.

Tumbili hao wa Borne huorodheshwa kama wanaoangamia na shirika la kitaifa la uhifadhi wa asilia IUCN.

Idadi yao ilipungua kwa takriban asilimia 60 kati ya 1950 na 2010 kutokana na uharibifu wa mazingira yao na uwindaji haramu na kushuka zaidi kwa asilimia 22 kunatarajiwa kati ya 2010 na 2025, kulingana na shirika hilo.


Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua yake ishara kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na wanakijiji waliomkamata